Picha 41: UZINDUZI WA FILAMU FUPI YA SAUTI YA KUNESE - SAUTI YA MTOTO MJANE MKOANI SHINYANGA

SHIRIKA lisilo la kiserikali la Monica Mhoja Edutainment Centre (MoMEC) lenye makao yake makuu jijini Dar es Salaam kwa kushirikiana na  shirika la Agape Aids Control Programme (AGAPE) na Paralegal Aid Centre Shinyanga limezindua Filamu Fupi ya SAUTI YA KUNESE -Sauti ya Mtoto Mjane. Mwandishi wetu Kadama Malunde anaripoti.


Uzinduzi huo umefanyika leo mjini Shinyanga katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa kutetea haki za watoto.

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Shinyanga Glory Mbiya aliyemwakilisha mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack.

 Filamu ya Sauti ya Kunese imeongozwa na Edgar Ngelela wa Keen Insights Production ambaye ni mtaalamu wa Sanaa MoMEC akisaidiana na Dr. Monica Mhoja Magoke ambaye ni mtaalamu wa masuala ya sharia na haki za binadamu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa filamu hiyo mkurugenzi wa MoMEC, Dakta Monica Mhoja Magoke alisema filamu hiyo inahusu ndoa za utotoni za kulazimishwa,kutothaminiwa kwa ustawi wa mtoto katika masuala ya elimu,ukatili wa kijinsia kama ukeketaji na unyanyasaji,mfumo dume katika maamuzi,kudhulumiwa mali mjane mtoto na watoto wake.

Alisema uzinduzi huo  wa filamu ni katika utekelezaji wa kampeni ya  kukomesha ukatili kwa mtoto mjane sambamba na uzuiaji wa ndoa katika umri mdogo mkoani Shinyanga.

Aliongeza kuwa kampeni hiyo itaendeshwa kwa njia ya uoneshaji filamu vijijini iliyopewa jina la Sauti ya Kunese ambayo italenga kuzungumzia na kuonesha madhara anayoyapata mtoto mjane baada ya kufiwa na mumewe huku wengi wao wakipoteza haki ya urithi kutokana na umri mdogo walionao.


Alisema uamuzi wa kuendesha kampeni hiyo unatokana na utafiti uliofanyika mwaka 2013 na ufuatiliaji wake mnamo mwaka 2015.

Akifafanua alisema katika utafiti uliofanyika ilibainika kuna kundi kubwa la watoto wa kike ambao hivi sasa ni wajane baada ya kufiwa na wanaume waliokuwa wameozeshwa ambao hivi sasa wanafanyiwa ukatili na familia za waliokuwa waume zao.

“Dhamira yetu ni kuelimisha, kuhamasisha na kuwajengea uwezo wanawake na wanaume kupinga ukatili wa kijinsia, ndoa za utotoni, ukiukwaji wa sheria na haki za binadamu kwa kutumia sanaa zenye kuelimisha na kuburudisha”,alisema Dr. Mhoja.

“Kupitia filamu ya Sauti ya Kunese tunaamini jamii itabadilika na kuachana na mila zilizopitwa na wakati kuhusu unyanyasaji wa wajane hususani wajane watoto, na tumebaini watu wengi wanaposikia neno mjane, wanaelewa ni wanawake watu wazima, kumbe wapo hata watoto wajane,” alieleza.

Akifafanua zaidi alisema suala la watoto wajane halitiliwi maanani na watu wengi na kwamba kupitia filamu itakayozinduliwa kwa kushirikiana na mashirika ya AGAPE na PACESHI ya mkoani Shinyanga jamii itapata elimu ya kutosha na kuelewa madhara yanayowakumba watoto hao na hivyo kushiriki kwa pamoja kupiga vita ndoa za utotoni.

Chanzo cha kupatikana kwa watoto wajane ni ndoa za utotoni, mkoa wa Shinyanga kwa mujibu wa tafiti mbalimbali ikiwemo za Shirika la Kimataifa la UNESCO unatajwa kuongoza kwa ndoa hizi, hivyo pamoja na kampeni na kukomesha ukatili kwa mtoto mjane, pia tutaelimisha jamii iache tabia ya kuozesha watoto wadogo,” alieleza.

Naye Afisa  Maendeleo ya jamii mkoani Shinyanga  Gloria Mbiya  aliyekuwa mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga,aliwataka watendaji wa vijiji,kata na halmashauri za wilaya kuhakikisha maeneo yao hakuna mtoto wa kike atakaye ozeshwa umri mdogo  au kutopatiwa elimu.

Tazama Picha 41 hapa chini matukio yaliyojiri wakati wa uzinduzi wa  Filamu ya Sauti ya Kunese

Mgeni rasmi Afisa  Maendeleo ya jamii mkoa wa Shinyanga  Gloria Mbiya  aliyemwakilisha  mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akizungumza wakati wa uzinduzi wa Filamu ya Sauti ya Kunese katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga leo Jumanne Januari 10,2017-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Mgeni rasmi Afisa  Maendeleo ya jamii mkoa wa Shinyanga  Gloria Mbiya akizungumza ukimbini.Kulia ni Afisa utamaduni mkoa wa Shinyanga Mariam Ally.Kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Stephen Magoiga
Kushoto ni Naibu meya wa manispaa ya Shinyanga Agnes Machiya akiwa na mtengenezaji wa Filamu ya Sauti ya Kunene Jessica  Chunny Magoke
Meneja Miradi shirika la PACESH John Shija akiimba wimbo wakati wa uzinduzi wa filamu ya Sauti ya Kunese
Wadau wa haki za watoto wakiwa ukumbini
Mkurugenzi wa shirika la MoMEC Dr. Monica Mhoja akizungumzia filamu ya Sauti ya Kunese ambapo alisema inagusia ndoa za utotoni za kulazimishwa,kutothaminiwa katika masuala ya elimu,ukatili wa kijinsia,mfumo dume katika maamuzi,kudhulumiwa mali  mjane mtoto na watoto wake
Wadau wa  watoto wakiwa ukumbini
Mkurugenzi wa shirika la MoMEC Dr. Monica Mhoja akisisitiza juu ya umuhimu wa jamii kuwaibua wajane watoto katika jamii ili waweze kusaidiwa 
Muongozaji (Director) wa filamu fupi ya Sauti ya Kunese Edgar Ngelela akielezea umuhimu wa  sanaa katika jamii ambapo alisema sanaa siyo uhuni bali ni kazi kama zilivyo kazi zingine na kusisitiza kuwa ili msanii afanikiwe anahitaji kuwa na Kipaji,bidii na elimu ya kutosha
Muongozaji wa filamu fupi ya Sauti ya Kunese Edgar Ngelela ambaye ni mtaalam wa sanaa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam akizungumza ukumbini
Mtengenezaji wa Filamu ya Sauti ya Kunene Jessica  Chunny Magoke akizungumza ukumbini
Rachel Kalile Masha afisa ustawi wa jamii MoMEC Dar es salaam
Diwani wa viti maalum katika manispaa ya Shinyanga Zainab Kheri (Chadema) akifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu Stephen Magoiga akizungumza ukumbini
Mkurugenzi wa shirika la PACESH Perpetua Magoke akizungumza ukumbini.Kulia ni mkurugenzi wa shirika la AGAPE John Myola.Kushoto ni mkurugenzi wa shirika la MoMEC Dr. Monica Mhoja
Watoto wakiwa ukumbini 
Wadau wa watoto wakiwa ukumbini 
Mgeni rasmi Glory Mbiya akikata utepe kuashiria uzinduzi wa filamu ya Sauti ya Kunese 
Mgeni rasmi Glory Mbiya akikata utepe kwenye CD ya filamu ya Sauti ya Kunese
Uzinduzi ukiendelea
Muigizaji katika filamu ya Sauti ya Kunese akipokea cheti cha utambuzi kwa kushiriki kikamilifu katika kufanikisha kupatikana kwa filamu hiyo
Mgeni rasmi akikabidhi cheti kwa muigizaji  Mussa Mombo
Muigizaji Stephen Almas akipokea cheti
Muongozaji wa filamu fupi ya Sauti ya Kunese Edgar Ngelela akipokea cheti
Muongozaji wa filamu fupi ya Sauti ya Kunese Edgar Ngelela akishikana mkono na mtengenezaji wa filamu hiyo Jessica Chunny Magoke
Afisa ustawi wa jamii MoMEC Rachel Kalile Macha akipokea cheti
Mkurugenzi wa shirika la AGAPE John Myola akipokea cheti

Mhusika mkuu katika Filamu ya Sauti ya Kunese Mary Simon Sweya "Kunese" akipokea cheti
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu Stephen Magoiga akizungumza ukumbini
Tunafuatilia kinachoendelea ukumbini
Mtengenezajiwa filamu fupi ya Sauti ya Kunese na muigizaji Mussa Momba wakifurahia jambo 
Waigizaji katika filamu ya Sauti ya Kunese wakijitambulisha 
Waigizaji wakiwa ukumbini
Waigizaji katika filamu ya Sauti ya Kunese wakiwa ukumbini 
Mgeni rasmi Glory Mbiya akiwa ameshikilia CD ya Filamu ya Sauti ya Kunese
Picha ya pamoja,mgeni rasmi,maafisa kutoka shirika la MoMEC,PACESH na AGAPE,watoto 
Picha ya pamoja wadau mbalimbali wa watoto
Picha ya pamoja na waigizaji katika filamu ya Sauti ya Kunese
Picha ya pamoja 
Picha ya pamoja
Picha ya pamoja
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post