NABII AWANYWESHA WAUMINI KEMIKALI YA KUSAFISHIA INJINI AKIDAI INA LADHA YA ASALI ILI KUTAMBUA MAPEPO MWILINI

Mtu mmoja anayejiita Nabii nchini Afrika Kusini amezua taharuki baada ya picha kusambaa kwenye mitandao ya kijamii zikimuonyesha akiwanywesha waumini wake kemikali ya kusafishia injini na kusema kuwa ina ladha kama asali.


Nabii Theo Bongani Maseko wa kanisa la Breath of Christ Ministries lililopo mjini Johannesburg amesema kuwa kemikali hiyo inashambulia virusi ndani ya mwili wa binadamu na kutambua mapepo.


Maseko alisema kuwa unywaji wa kemikali hiyo hauna madhara yoyote kiafya kwani yeye mwenyewe amewahi kunywa.


“Ina ladha kama asali, nimewahi kunywa mara mbili” alisema Maseko.

Aidha, alisema kuwa waumini wake wote ambao tayari wameshatumia dawa hiyo hakuna hata mmoja aliyepata matatizo ya kiafya na kwamba wote wamekuja na ushuhuda wa kuponywa matatizo yao. Alisema kuwa Mungu alimpa wito huo kabla hata hajazaliwa.


Nabii huyu si yeye pekee aliyefanya vitu vya kushangaza kwani kuna mwingine alikuwa akiwapulizia waumini dawa ya kuuwa wadudu na mwingine akiwanywesha petroli.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post