MUME AUAWA KISHA KUTUPWA CHINI YA DARAJA BAADA YA KUMALIZA KUNYWA POMBE NA WAKE ZAKE WAWILI

NB-Siyo daraja katika habari hapa chini
MKAZI wa kijiji cha Sakalilo kilichopo mwambao wa Ziwa Rukwa wilayani Sumbawanga, Kalitus Jacob (44) ameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kisogoni kisha mwili wake ukatupwa chini ya daraja la Mumba na watu wasiojulikana.


Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, George Kyando alisema tukio hilo lilitokea Januari 16 mwaka huu, saa 12:00 jioni katika kijiji cha Sakalilo “Kabla ya tukio, alionekana akiwa kilabuni na wake zake wawili wakinywa pombe, aliwaaga na kuondoka na hakurudi tena hadi alipokutwa akiwa amekufa.

 Chanzo cha mauaji hakijajulikana na juhudi za Jeshi la Polisi zinaendelea ili kubaini kiini cha mauaji hayo,” alieleza Kamanda Kyando.

Alisema kuwa mwili wa marehemu umekabidhiwa kwa ndugu zake kwa ajili ya maandalizi ya maziko yake baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu.

Alisema watuhumiwa hawajakamatwa huku uchunguzi unaendelea ili kuweza kuwabaini waliohusika katika mauaji hayo.
IMEANDIKWA NA PETI SIYAME,-HABARILEO SUMBAWANGA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post