MUME AUA MKE NA MTOTO,AJARIBU KUJIKATA SEHEMU ZAKE ZA SIRI BAADA YA KUAMBIWA ANA MCHEPUKO

Mkazi wa Bukene wilayani Nzega mkoani Tabora, amemuua mkewe pamoja na mtoto wake.


Mkazi huyo Rashid Nassoro, baada ya kuwaua watu wake wa karibu alikimbia na baadae kujaribu kujiua kwa kujichoma kisu tumboni na kujaribu kukata sehemu zake za siri.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Khamis Selemani amethibitisha tukio hilo na kusema lilitokea juzi eneo la Bukene, wilayani hapa baada ya Rashid Nassoro (22) kumuua mkewe kwa kumchoma visu tumboni.


Alisema, baada ya kumuua mke wake, Rashid alimnyonga mtoto wake wa miezi minne na kukimbia.


Kamanda Selemani, alisema baada ya kukimbia Rashid aliamua kutaka kujiua kwa kujichoma kisu tumboni na kujaribu kukata sehemu zake za siri.


Alisema chanzo cha tukio hilo ni mwanamke kumtuhumu mume wake kuwa ana uhusiano na mwanamke mwingine jambo lililomchukiza mwanaume huyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post