MBWA AMEZA KISU,AFANYIWA UPASUAJI


Mbwa ambaye alimeza kisu cha urefu wa sentimita 20 anapata nafuu baada ya kufanyiwa upasuaji.
Mbwa huyo wa umri wa wiki 12 kwa jina Macie, alikimbizwa kwa daktari wa mifugo kwa huduma ya dharura baada ya kuanza kukohoa.

Mwenye mbwa huyo anasema alidhani kuwa alikuwa amemeza kifaa cha kuchezea cha watoto, lakini X ray baadaye ilionyesha picha ya kisu kikuwa tumboni.

Daktari ambaye amekuwa akimtunza mbwa huyo tangu afanyiwe upasuaji anasema ana bahati sana kuwa hai.

Mwenye mbwa huyo kutoka Glasgow alikuwa amempoteza mbwa wake mwingine kutokana na ugonjwa wa saratani

Siku moja baada ya kufanyiwa upusuaji alionekana mchangamfu. Mbwa huyo amekuwa akirudishwa kwa daktari kufanyiwa ukaguzi kwa muda wa wiki mbili na sasa anaendelea kupata nafuu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post