Picha: TRENI YA MWENDO WA HARAKA - DELUX YAANGUKA PWANI IKITOKA KIGOMA KWENDA DAR ..TAZAMA PICHA


TRENI ya mwendo haraka, (DELUX), iliyokuwa ikitokea Kigoma kwenda jijini Dar es Salaam, imeanguka eneo la Ruvu mkoani Pwani leo Jumapili Januari 29, 2017.

Msemaji wa TRL, Medladjy Maez amesema treni hiyo imeanguka leo majira ya saa 9:40 alasiri. 

"Treni yetu ya Deluxe ilipokuwa ikirejea Dar kutoka Kigoma imepata ajali kati ya vituo vya Ruvu na Ngeta ambapo mabehewa 9 yamepata ajali",amesema 

Amesema kati ya hayo manne yameanguka, mawili yametenguka na matatu yameacha njia..

Inaelezwa kuwa watu kadhaa wamepata majeraha mepesi isipokuwa mmoja ndiye aliyepata majeraha makubwa na amekimbizwa hospitali kwa matibabu zaidi.

Habari na Khalfan Said wa K-VIS BLOG


Treni ikiwa imeanguka

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post