BASI LA BENY JUNIOR LAPATA AJALI LIKIKATA KONA STENDIYA LUDEWA

Watu kadhaa wamejeruhiwa katika ajali baada ya Coaster /basi la Beny Junior linalofanya safari zake kati ya Lugarawa na Ludewa kupata ajali eneo la stendi ya Ludewa mkoani Njombe.

Ajali hiyo imetokea majira ya saa 5 asubuhi wakati basi hilo likijaribu kukata kona kuingia stendi ya Ludewa mjini.

Dereva wa basi hilo amekimbia na kutelekeza basi hilo huku majeruhi wamekimbizwa hospitali ya Wilaya ya Ludewa kwa matibabu zaidi .

Jitihada za kumtafuta kamanda wa polisi wa mkoa wa Njombe zinaendelea

CHANZO-http://www.matukiodaima.co.tz/

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post