ASKARI POLISI MWENYE MKE AJINYONGA TABORA KISA 'MCHEPUKO WAKE' KUWA NA MCHEPUKO MWINGINEAskari aliyekuwa akifanya kazi kituo kidogo cha polisi tarafa ya Igurubi wilayani Igunga mkoani Tabora, amejiua kwa kujinyonga kwa kutumia shuka kutokana na kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.


Askari aliyejiua ametambulika kwa jina la G.4185 PC Geofrey Mwenda (32 ) ambaye inadaiwa hawara yake mpya ndiyo chanzo cha kuchukua maamuzi ya kutoa uhai wake.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Hamisi Issa alisema tukio hilo limetokea juzi saa tatu usiku.


Akisimulia tukio hilo, Kamanda Issa alieleza kuwa askari huyo baada ya mke wake kusafiri, aliamua kuchukua uamuzi ya kuwa na mpenzi wa nje.


Alieleza askari huyo baadaye alikuja kugundua mpenzi wake ambaye hakuweza kumtaja jina lake, kuwa alikuwa na mwanaume mwingine mbali ya askari huyo.


Kutokana na ugunduzi huo ambao ulimfanya askari huyo achukie ndio alipoamua kujiua kwa kujinyonga kwa kutumia shuka na kujining’iniza kwenye mti.

Na Robert Kakwesi, Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post