WASIRA: SIJATEULIWA KUWA MSEMAJI WA CCM


Aliyekuwa Waziri na Mbunge wa Jimbo la Bunda, Stephen Wasira, amesema kuwa taarifa zilizozagaa  kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa ameteuliwa kuwa msemaji wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) sio za kweli.

Taarifa hiyo imedai kuwa Wasira ameteuliwa kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Christopher Ole Sendeka aliyeteuliwa na Rais Magufuli kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe huku nafasi ya mweka hazina na Naibu Katibu Zanzibar zikidaiwa kupata viongozi wapya.

Wasira amesema kuwa taarifa hizo sio za kweli na ni uzushi tu wa watu ambao wana nia mbaya na hawamtakii mema.Pia CCM kupitia ukurasa wao wa Twitter alikanusha taarifa hizo

“Zipuuzeni hizo taarifa, hakuna kitu kama hicho, nmepigiwa simu na watu wengi sana wanaulizia suala hili. Na sijui kuna ajenda gani nyuma ya hawa waliozusha” Amesema Wasira.

Wasira amekuwa mwanachama wa CCM kwa muda mrefu huku akishika nyadhifa mbali mbali, ingawa mwaka 1995,alikihama chanma hicho na kujiunga na NCCR-Mageuzi baada ya kuangushwa kwenye kura za maoni za ndani ya CCM na Jaji Joseph Sinde Warioba.

Taarifa inayosambazwa kwenye mitandao kuhusu uteuzi wa wajumbe wa Sekretarieti sio sahihi. Kamati Kuu haijafanya uteuzi wa mjumbe yeyote.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post