MWANZILISHI WA MTANDAO WA JAMIIFORUMS MAXENCE MELO AACHIWA KWA DHAMANA


Mwanzilishi wa mtandao wa JamiiForums Maxence Melo ameachiwa kwa dhamana leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya kukaa mahabusu kwa takribani siku 5.


Melo anakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kumiliki na kuendesha tovuti ambayo haijasajiliwa hapa nchini Tanzania (JamiiForums).


Mashtaka mengine ni kuzuia na kuharibu taarifa ambazo Jeshi la Polisi wamekuwa wakizitaka kwa ajili ya uchagunguzi chini ya kifungu cha 22 cha Sheria ya Makosa ya Mitandao na kushindwa kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi na kuharibu uchunguzi chini ya kifungu cha namba 22 cha Sheria ya Makosa ya Mitandao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post