MWANDISHI WA HABARI PAUL KAYANDA AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA AGIZO LA DC KAHAMA

Paul Kayanda akipanda kwenye gari la polisi leo Ijumaa Desemba 30,2016
Mwandishi wa habari mkoa wa Shinyanga Paul Kayanda amefikishwa mahakamani kwa agizo la Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkulu kwa madai kuwa mwandishi huyo wa habari anamchafua kwa njia ya email.

Mwandishi huyo anadaiwa kuandika habari kuhusu mkuu huyo wa wilaya kuibiwa laptop mbili nyumbani kwake kisha kuwaweka ndani/polisi kwa muda wa siku saba watu watatu akiwemo kijana anayeishi naye nyumbani bila kuwafikisha mahakamani.

Mwandishi huyo alikamatwa leo asubuhi kisha kufikishwa katika mahakama ya wilaya kisha kurudishwa tena polisi kutokana na kukosekana kutokuwepo kwa shtaka lolote lililofunguliwa kutoka polisi kwenda mahakamani.

Hata hivyo baada ya kurudishwa polisi,alifikishwa katika wilaya ya Mwanzo  wilayani humo na kusomewa mashtaka ya kumchafua mkuu huyo wa wilaya kisha kuachiwa kwa dhamana na kutakiwa kurudi mahakamani  Januari 02,2017.

Mkuu huyo wa wilaya amesema mwandishi wa habari huyo amefikishwa mahakamani kutokana na kuandika habari za kumchafua kwa kusambaza habari kupitia email na kumtumia sms alizodaiwa siyo za maadili.

                                      TAARIFA KWA UMMA
Uongozi wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (SPC) umefuatilia kwa undani suala la mwandishi wa habari Paul Kayanda kufikishwa mahakamani kwa agizo la mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu kwa kile kinachotajwa kuwa ameandika habari za kumchafua baada ya mkuu huyo wa wilaya kuibiwa laptop mbili nyumbani kwake.

Uongozi wa klabu umefanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo mkuu huyo wa wilaya ya Kahama lakini pia na mwandishi Paul Kayanda kuhusu suala hilo.

Kutokana na suala hilo kuwa na utata tumekubaliana kesho Jumamosi Desemba 31,2016 saa tano asubuhi,uongozi wa klabu ya waandishi wa habari,waandishi wa habari walioko wilayani Kahama na mkuu huyo wa wilaya  tutakutana katika kikao cha pamoja kwa ajili ya kuzungumzia suala hilo na kutafuta utatuzi wake hivyo yatakayojiri tutawatarifu.

Imetolewa na
Kadama Malunde
Mwenyekiti SPC



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527