LOWASSA AFUNGUKA KUHUSU FIDEL CASTROL,ASEMA KUWA NI SHUJAA WAKE WA DUNIA

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Edward Lowassa amesema kuwa aliyekuwa Rais wa Cuba na mwana mapinduzi wa nchi hiyo, Fidel Castro alimhamasisha kuingia katika uongozi.

Ameyasema hayo alipotembelea ubalozi wa Cuba hapa nchini kutoa pole na kusaini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Castro kilichotokea Novemba 25 mwaka huu jijini Havana nchini Cuba.

Lowassa amesema Marehemu Castro alikuwa mwana mapinduzi na ni miongoni mwa wanasiasa waliomhamasisha kuingia kwenye uongozi kutokana na alivyokuwa akiwatetea masikini na wanyonge duniani, hali ambayo imelisababishia taifa hilo dogo kuogopwa kutokana na uimara wake.

“Castro alikuwa kiongozi imara sana,kila kiongozi makini lazima awe  kinara wa kuwatetea wanyonge na masikini popote walipo”alisema Lowassa.

Lowassa amesema kuwa Castro aliifanya Cuba pamoja na udongo wake uitikise dunia kwa kuwa kila mahali ukienda ni lazima utasikia jina la Castro.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post