KESI YA MKURUGENZI WA JAMII MEDIA MAXENCE MELO YAPIGWA KALENDA

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es salaa leo, Desemba 29, 2016 imeahirisha kusikiliza kesi inayomkabili Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jamii Media, ndugu Maxence Melo hadi January 26, 2017 kufuatia upande wa Jamhuri kudai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Maxence Melo anashtakiwa kwa makosa matatu ikiwemo kuzuia Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi kwa mujibu wa Sheria ya Makosa ya Mtandao na Kusajili tovuti ya JF kwa kikoa cha .com badala ya .co.tz jambo ambalo Serikali inadai ni kinyume cha sheria.

Kutoka kushoto ni Wakili wa kampuni ya Jamii Media Benedict Ishabakaki, Maxence Melo Mkurugenzi mtendaji wa Jamii Media, Mbaraka Islam wa Raia Mwema na Wakili wa kampuni ya Jamii Media Jebra Kambole, wakiwa katika viunga vya Mahakama ya Kisutu.

Mashauri yote ya kesi hiyo yameahirishwa huku shauri la tovuti kutosajiliwa kwa kikoa cha .co.tz,Mheshimiwa Hakimu Simba anyaeendesha shauri hilo ameutaka upande wa Jamhuri kufanya upelelezi haraka kwa shauri hilo.

Maxence Melo, aliachiwa kwa dhamana Desemba 19, 2016 Mahakamani hapo baada ya kukaa lupango kwa siku kadhaa mpaka alipokidhi vigezo na masharti ya kudhaminiwa ambapo mahakama ilimtaka arudi leo kusikiliza kesi yake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post