WAKUU WA MIKOA SABA HATARINI KUTUMBULIWA...WAMEKALIA KUTI KAVU

Wakuu wa mikoa saba wamekalia kuti kavu kutokana na kushindwa kutekeleza agizo la Rais John Magufuli kumaliza tatizo la madawati katika mikoa yao.


Akizungumza jana wakati akipokea madawati 3,500 yenye thamani ya Sh300 milioni kutoka benki ya NMB, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais -Tamisemi, George Simbachawene alisema mikoa ya wakuu hao saba inayoongoza kwa upungufu wa madawati ni Geita, Mwanza, Kigoma, Mara, Rukwa, Simiyu na Dodoma.

Simbachawene alisema kutokana na kushindwa kutekeleza ahadi hiyo ametoa siku 43 na wasipotekeleza watakuwa wameshindwa kwenda na kasi ya Dk Magufuli.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post