RAIS MAGUFULI AMTEUA ALIYEKUWA KIGOGO WA POLISI KUWA KATIBU TAWALA WA MKOA WA KAGERA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 18 Novemba, 2016 amemteua aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Bw. Diwani Athuman kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera.Uteuzi wa Bw. Diwani Athuman unaanza mara moja.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Wenyeviti wa Bodi katika taasisi tano za Serikali kama ifuatavyo.

Kwanza, Rais Magufuli amemteua Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jaji Joseph Sinde Warioba kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA)

Uteuzi huu umeanza tarehe 16 Novemba, 2016.

Pili, Rais Magufuli amemteua Dkt. Jones A. Kilimbe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na amemteua Bw. Sylvester M. Mabumba kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Uteuzi huu umeanza tarehe 17 Novemba, 2016

Tatu, Rais Magufuli amemteua Prof. Patrick Makungu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Uhandisi na Usanifu Mitambo (TEMDO).

Uteuzi huu umeanza tarehe 16 Novemba, 2016.

Nne, Rais Magufuli amemteua Bw. Martin Madekwe kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Fidia ya Ardhi.

Uteuzi huu umeanza tarehe 17 Novemba, 2016.

Tano, Rais Magufuli amemteua Prof. Raphael Tihelwa Chibunda kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wakurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya Kitropiki Tanzania (TPRI)

Uteuzi huu umeanza tarehe 17 Novemba, 2016.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

18 Novemba, 2016

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post