MHADHIRI CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (UDSM) AONDOKA NA MTOTO ALBINO SHINYANGA

Novemba 28,2016,hapa ni katika kituo cha Buhangija mkoani Shinyanga-Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Emmanuel Shemaghembe (pichani) amejitolea kuishi na kumsomesha mtoto mwenye ulemavu wa ngozi Suzana Malale(03) aliyekuwa analelewa katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wa ngozi Buhangija katika manispaa ya Shinyanga baada ya watu 65 wenye ulemavu wa ngozi waliokuwa wanalelewa kituoni hapo kurudishwa katika familia zao. 

Kwa mujibu wa Mkuu wa kituo cha Buhangija Seleman Kipanya watu wenye ulemavu wa ngozi waliorudishwa katika familia zao ni 65 kati yao 12 ni watoto wenye umri chini ya miaka minne na watoto wenye ualbino waliopo kituoni sasa ni 174,wasiosikia 61 na wasioona 24.

Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Kushoto ni Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Emmanuel Shemaghembe,katikati ni msimamizi mkuu wa kituo cha Buhangija mwalimu Seleman Kipanya,kulia ni diwani wa kata ya Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga Emmanuel Ntobi (Chadema) wakibadishana mawazo wakati mhadhiri huyo alipofika kituoni hapo kumchukua mtoto Suzana Malale baada ya kufuata taratibu zote za kiserikali kuwa mfadhili wa mtoto huyo.Shemaghembe alitoa wito kwa watanzania kujitokeza kuwasaidia watoto wenye ulemavu kwani wengi wao wanaishi katika mazingira magumu na hatarishi.
Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Emmanuel Shemaghembe akizungumza katika kituo cha Buhangija ambapo alisema ameguswa na maisha ya watoto hao hivyo familia yake imejitolea kuishi na mtoto Suzana Masele (03),na atakwenda naye jijini Dar es salaam kwa ajili ya kumlea kumsomesha 
Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Emmanuel Shemaghembe alisema mtoto Suzana ataanza masomo yake Desemba 06,mwaka huu katika shule yake ya Bubble Guppies iliyopo Goba jijini Dar es salaam

Kushoto ni Diwani wa kata ya Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga Emmanuel Ntobi akiwa amembeba Mtoto Suzana anayetoka wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, ambaye ni miongoni mwa watoto 65 wenye ualbino waliokuwa kwenye kituo cha Buhangija waliorudishwa nyumbani na serikali ili wakajichanganye na jamii
Diwani wa kata ya Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga Emmanuel Ntobi akiwa amembeba Mtoto Suzana.Ntobi ni rafiki yake na Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Emmanuel Shemaghembe tangu akiwa mwanafunzi katika chuo hicho na alifundishwa na mhadhiri huyo na wamekuwa marafiki mpaka sasa
Shemagembe aliahidi kumchukua na kumsomesha mwanafunzi mwenye ualbino atakayefanya vizuri katika mtihani wa darasa la saba mwaka 2017 na atakayefanya vizuri katika mtihani wa kidato cha nne mwaka 2017. 
Mkuu wa kituo cha Buhangija Seleman Kipanya akizungumza,ambapo alisema mhadhiri huyo wa chuo cha Dar es salaam Emmanuel Shemaghembe amefuata taratibu zote za kiserikali na kukutana na wazazi wa mtoto huyo na kufanikiwa kumchukua mtoto Suzana Malale kwa ajili ya kumlea na kumsomesha. Alisema mchakato wa mhadhiri huyo kuwa mfadhili wa mtoto huyo ulianza tangu mwezi Agosti mwaka huu baada ya mhadhiri huyo kufika kituoni hapo akitekeleza mradi wa UNESCO
Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Emmanuel Shemaghembe akiwa amembeba mtoto wake Suzana Malale
Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Emmanuel Shemaghembe akiwa katika picha ya pamoja na watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija
Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Emmanuel Shemaghembe akifurahia kuwa na watoto
Diwani wa kata ya Ngokolo Emmanuel Ntobi naye akaungana na rafiki yake Emmanuel Shemaghembe kupiga picha ya pamoja na watoto
Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Emmanuel Shemaghembe akiwa na mtoto Suzana
Baadhi ya walimu walezi wa watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija wakimuaga mtoto Suzana
Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Emmanuel Shemaghembe akibadilishana mawazo na mmoja wa vijana waliopo katika kituo cha Buhangija.

Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527