Makubwa haya: BIBI AMLAZIMISHA MJUKUU WAKE KUTAFUNA KINYESI


Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Amina Hamisi (56) mkazi wa mtaa wa mahina kata ya Butimba Jijini Mwanza, anashikiliwa na polisi baada ya kumlazimisha mjukuu wake wa kike  (jina linahifadhiwa) mwenye umri wa miaka 7 kula kinyesi.


Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Kamishina Msaidizi wa Polisi Augustino Senga amedai kuwa tukio hilo limetokea Novemba 11, mwaka huu ambapo mtoto huyo alikwenda chooni kujisaidia na kushindwa kumwagia maji ili kuondoa kinyesi chake ndipo bibi yake ili kumuadhibu alimuamuru kula kinyesi hicho kitendo ambacho mtoto huyo alikitekeleza.


Baada ya tukio hilo kutokea raia wema walitoa taarifa polisi ambao walifika eneo la tukio na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo.


Kamanda Senga ametoa wito kwa wakazi wa jiii la Mwanza kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kudhibiti vitendo vya kikatili hasa kwa watoto wadogo na kuongeza kuwa ukatili ni kosa kisheria hivyo wananchi waache kufanya vitendo hivyo na watakao bainika sheria itachukua mkondo wake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post