Sambamba
na hilo, amewaonya wabunge wa upinzani, kuacha kuwatumia vibaya
wananchi na kuwachonganisha na Rais wao, baada ya kuona wamebanwa kulipa
kodi.
Mbunge
huyo alitoa onyo hilo jana wakati akichangia Mapendekezo ya Mpango wa
Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2017/2018 na Mwongozo wa kuandaa mpango wa
bajeti ya serikali kwa mwaka 2017/2018 uliowasilishwa juzi na Waziri wa
Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango.
“Nyinyi
mawaziri ni abiria na mmekaa siti za mbele kwenye gari analoendesha
Rais Magufuli msimkimbize, baadhi yenu msimpotoshe rais yeye si mchumi
mtamletea matatizo mbeleni, pesa zimepotea si kwa sababu zimefichwa
kwenye magodoro ila zimepotea kwa sababu pesa zote zimewekwa Benki Kuu
ya Tanzania (BoT), zitoeni pesa hizo ziende kwenye mabenki,” alisema.
Alisema Bunge limepoteza mwelekeo, limekuwa la kulialia na kumlaumu Rais Magufuli kwa sababu amebana wakwepa kodi na kufafanua “Rais
aliliomba Bunge hili limsaidie kutumbua majibu, tumsaidie mipango ya
serikali iweze kutekelezeka ili kujenga nchi yetu, najua Rais ana nia
njema na nchi, Hapa Kazi Tu inawafanya wafanyabiashara waliozoea kukwepa
kodi wamebanwa sasa wanalia biashara imekufa, watumishi waliozoea posho
za hapa na pale, kusafiri wamebanwa, wabunge tuliozoea kula andazi la
inchi 18 sasa tunakula la sentimita mbili, kwenye kamati tumebanwa
posho, tunalialia kisa tumeshikwa pabaya na kuwaingiza wananchi wanyonge
eti hawana pesa.
"Kiongozi
wa Upinzani, Freeman Mbowe umepewa gari na serikali na mafuta
unawekewa, yamejaa kwenye gari, kiyoyozi kipo saa 24 unasema serikali
imefilisika huku unawachonganisha wananchi na Rais wao, unawatumia
vibaya wananchi, Msigwa kama Mchungaji (Peter, Mbunge wa Iringa Mjini)
tumia taaluma yako kuwashauri wenzako wawe kwenye safari hii... Rais
Magufuli anatupeleka Kaanani kuishi maisha mazuri, ametupandisha basi
kutupeleka nchi ya ahadi.
"Nashauri
anapoendesha gari ajue kuna matuta, akiendesha vibaya Watanzania
atatuangusha, kuna zebra na wanafunzi wanavuka, akiona spidi iko 50
apunguze mwendo... na nyinyi mawaziri mmekaa siti za mbele za gari la
Rais, msimpotoshe”, alifafanua.
Mbunge
wa Mtera, Livingstone Lusinde(CCM) alisema ni lazima uchumi unapokua,
uoneshe kwenye maisha ya wananchi wa vijijini ; na si kuonesha ujuaji wa
pointi kwenye makaratasi.
Alisema “Upinzani
msizunguke kusema serikali imefilisika, semeni ukweli, Mbowe
umefilisika, umeshindwa kulipa madeni, serikali haijafilisika, inalipa
mishahara, inalipa madeni yake”.
Naye
Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya (Chadema) alisema kila sehemu kuna
njaa, mtaani wananchi wanalia hakuna pesa na hata wabunge wamepauka kwa
kukosa fedha.