JESHI LA POLISI LAZUNGUMZIA KIFO CHA BONDIA THOMAS MASHALI


JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema kuwa wanaendelea na upelelezi kufuatia kuuawa kwa mwanamasumbwi Thomas Mashali na watatoa taarifa ya kifo hicho siku ya Jumatano.

Akizungumza na waandshi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro alisema taarifa zilizopo kufuatia kifo cha bondia huyo ni za kufikirika na zinasemwa tu, hivyo Jumatano atatoa taarifa hiyo.

Kamishina Sirro alisema kuwa bondia huyo ni mtu mkubwa na hakuna mtu aliethibitisha kuwa ni mny'ang'anyi, hivyo mpaka sasa ni maneno ya mtaani tu.

“Mimi ndio napata taarifa juu ya kifo cha bondia huyo. Ngoja nisubiri taarifa niweze kutoa siku ya Jumatano, ambapo nitakuwa na majibu sahihi. Kwa leo niache tu”alisema Kamishna Sirro.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post