HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI YAPOKEA MSAADA WA MASHINE KUBWA YA KISASA YA UTRA SOUND KWA WAGONJWA WENYE MATATIZO YA FIGO


Hospitali ya Taifa Muhimbili imepokea msaada wa mashine kubwa na ya kisasa ya Utra Sound maalum kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wenye matatizo ya Figo.


Msaada huo umetolewa jana na Hospitali ya Chuo Kikuu cha Haukeland cha nchini Norway ambapo pamoja na mambo mengine wameahidi kuendelea kutoa ushirikiano katika maeneo ya elimu , utafiti pamoja na vifaa tiba.


Daktari Bingwa wa magonjwa ya Figo ambaye pia Mhadhiri kutoka MUHAS Paschal Ruggajo amesema mashine hiyo itasaidia kuchukua sampuli ya figo kwa ajili ya kugundua magonjwa ya Figo , kuweka vifaa kwenye mishipa damu kwa wagonjwa wanaoanzishiwa matibabu ya uchujaji wa damu na kugundua matatizo mbalimbali ya Figo.


“ Kwa muda mrefu sasa tumekua na ushirikiano wa karibu kati ya Hospitali hiyo , MUHAS na MNH na wametusaidia kufundisha Madaktari sita wa Figo , wameshatoa mashine za kusafisha Figo na sasa wametupatia mashine hii kubwa ya Utra Sound kwakweli tunawashukuru kwa msaada wao.” Amesema Dk. Ruggajo.


Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili , Dk . Hedwiga Swai ambaye ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba ameishukuru Hospitali hiyo ya Haukeland na kusisitiza kuwa msaada huo umekuja wakati muafaka kwakua mashine hiyo itasaidia sana katika kitengo cha Figo

Profesa Einar Svastard ( kulia) akimkabidhi msaada wa mashine kubwa ya kisasa ya Utrasound Mkurugenzi wa huduma za tiba MNH Dk. Hedwiga Swai .

Profesa Einar Svastard akimfanyia uchunguzi mgonjwa kwa kutumia mashine hiyo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post