MATOKEO YA MECHI ZA VPL:SIMBA SC WAIFUNGA MWADUI FC KWA MARA YA KWANZA


Ligi Kuu soka Tanzania bara msimu wa 2016/2017 iliendelea tena Jumamosi ya October 29 2016 kwa michezo mitano kupigwa katika viwanja vitano, macho ya mashabiki wengi wa soka la bongo walikuwa wana hamu ya kujua kama Simba ataifunga Mwadui FC kwa mara ya kwanza katika Ligi Kuu.


Mwadui FC walipanda daraja 2015 wakiwa na kocha wao Jamhuri Kiwelu ‘Julio’ ambaye kwa sasa amejiuzulu nafasi hiyo kutokana na kutoridhishwa na vitendo vya waamuzi, Mwadui FC kabla ya mchezo wa leo walikuwa wamecheza mara 2 na Simba wametoka sare mara moja na kuifunga Simba uwanja wa Taifa katika mchezo wa marudiano mara moja.



Leo October 29 2016 Simba imelipa kisasi ya kichapo cha goli 1-0 ilichofungwa May 8 2016 uwanja wa Taifa Dar es Salaam, goli likifungwa na Jamal Mnyate wakati huo akiwa Mwadui, leo Mohamed Ibrahim wa Simba amefanikisha Simba kuiadhibu Mwadui FC kwa magoli 3-0, magoli yakifungwa na Mohamed Ibrahim dakika ya 32 na 50 na kutoa pasi ya goli la Shiza Kichuya dakika ya 45.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post