MRITHI WA HANS VAN PLUIJM YANGA ATUA DAR ES SALAAM


 
Siku 14 baada ya klabu ya Dar es Salaam Young Africans kupitia kwa kaimu katibu mkuu wake Baraka Deusdedit atangaze kukanusha klabu hiyo kuwa na mpango wa kumfuta kazi Hans van Pluijm na kurithiwa na kocha wa Zesco United ya Zambia George Lwandamina, hatimae leo October 24 ukweli wa taarifa hizo umeanza kufahamika.


Yanga walikanusha kuwa katika mpango wa kumfuta kazi kocha Hans van Pluijm October 10 2016 lakini sasa ujio wa kuwasili kwa kocha mzambia George Lwandamina Dar es Salaam kunaanza maliza uvumi wa tetesi hizo, Lwandamina tayari yupo Dar es Salaam licha ya kuwa Yanga hawajathibitisha lolote.

Kwa tetesi na habari zinazosambaa katika mitandao ya kijamii zinaeleza kuwa kocha Lwandamina alishamalizana na Yanga na amesaini mkataba wa miaka miwili ya kumrithi kocha Hans van Pluijm.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post