MATOKEO YA MECHI ZA LIGI KUU SOKA TANZANIA BARA LEO JUMAMOSI 17.09.2016 - YANGA, SIMBA, AZAM

Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea tena Jumamosi ya Septemba 17, 2016 kwa michezo sita kuchezwa katika viwanja sita tofauti, moja kati ya mchezo uliochezwa ni Azam FC waliwakaribisha Simba katika dimba Uhuru Dar es Salaam, katika mchezo ambao kila mmoja alikuwa anawania kupata ushindi ili apate nafasi ya kuongoza.

Huu ulikuwa ni mchezo unazikutanisha timu ambazo zote zilikuwa na point 10 na wastani wa magoli ya kufunga na kushinda walikuwa wapo sawa, haukuwa mchezo rahisi kuona timu ikiruhusu kufungwa kwani hadi dakika ya 45 za kwanza zinamalizika walikuwa 0-0.

Kipindi cha pili dakika ya 67 Simba wakabadili ubao wa matokeo na kuufanya usomeke 1-0 baada ya Shiza Kichuya kufunga goli la ushindi kwa shuti kali lililomshinda golikipa wa Azam FC Aishi Manula, Simba sasa atashuka dimbani Septemba 24 kucheza dhidi ya Majimaji katika uwanja wa Uhuru, wakati Azam FC watakuwa Mtwara kucheza na Ndanda FC.

Matokeo ya michezo mingine ni;

Mbeya City 0 – 0 Prisons
Mtibwa Sugar 2 – 0 Kagera Sugar
Ruvu Shooting 0 – 4 Mbao FC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post