Mahakama Yaruhusu Mabinamu Kufanya Mapenzi...Aliyehondomola Tendo la Ndoa na Binamu Yake na Kufungwa Miaka 10 Aachiwa Huru

Mahakama ya juu nchini Kenya imehalalisha uhusiano wa kimapenzi baina ya mabinamu kwa sababu inakubalika katika baadhi ya jamii nchini humo.


Mahakama hiyo imemuachilia huru mtu mmoja aliyekuwa amefungwa kwa kosa la kushiriki ngono na binamu yake mwaka wa 2014 kwa sababu sio makosa nchini Kenya.

Jaji wa mahakama ya juu James Makau, alisema katika uamuzi kuwa kujamiana kwa maharimu sio haramu nchini Kenya.

''Ibara maalum inachoshughulikia ngono ya maharimu hajata binamu kuwa mmoja wa wale ambao kujamiana nao ni haramu maksudi, kwa sababu baadhi ya jamii nchini Kenya zinaruhusu sio tu ngono bali hata ndo baina yao''

Jaji wa mahakama ya juu James Makau, alisema katika uamuzi kuwa kujamiana kwa maharimu sio haramu nchini Kenya.

''Jamii ya wahindi, waislamu na baadhi ya makabila humuhumu Kenya hukubali ndoa baina ya mabinamu'' alisema jaji Makau.

Bwana huyo ambaye anatambulika kama WOO alikamatwa mwaka wa 2014 kwa kushiriki ngono na mpenzi wake wa kike ambaye pia ni binamu yake na akahukumiwa kifungo cha miaka 10 gerezani.

''Kwa ufupi hakuna ushahidi wowote uliotolewa kuthibitisha kuwa ngono baina ya wawili hao ni kinyume cha sheria na kwa sababu hiyo ninaamuru mtu huyo aachiwe huru mara moja'' hukumu ya jaji Makau.
 Via>>BBC SWAHILI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post