Wanafunzi Wawili wa Somo la Udaktari Watiwa Mbaroni Kwa Kumfanyia Ukatili MBWA

Polisi katika mji wa Chennai nchini India wamewatia mbaroni wanafunzi wawili wa somo la udaktari na kuwashtaki kwa makosa ya ukatili dhidi ya wanyama.

Haya yanajiri baada ya video kusambaa mitandaoni, inayoonyesha wanafunzi hao wakiamwangusha mbwa kutoka kwenye paa la nyumba.

Mwanafunzi mmoja anaonekana akimwangusha mbwa huyo huku mwingine akichukua video ya tukio hilo.

Video hiyo ilisambaa sana katika mitandao ya kijamii hadi walipokamatwa

Miito ya kuwakamata wanaume hao wawili ilitolewa baada ya Umaarufu wa video hiyo kwenye mitandao ya kijamii.

Mbwa huyo kwa sasa anatibiwa.

Wanafunzi hao wanakabiliwa na kifungo cha miaka mitano gerezani, na pia huenda wakanyimwa nafasiya kuwa madakatari.

Daktari mmoja wa mifugo ameviambia vyombo vya habari nchini India kuwa iwapo watapatikana na hatia huenda wakanyimwa leseni ya kuwa madaktari katika siku za usoni.
Via>>BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post