Video!! Kijana Apachikwa jina "Shabiki wa Mwendokasi" Baada ya Kumshangilia Kwa Aina Yake Rais Magufuli


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli hivi karibuni katika ziara zake alikutana na kijana aliyemshangilia kwa nguvu zake zote hali ambayo ilimfanya mkuu huyo wa nchi kumwita na kupiga naye picha.


Kijana huyo ambaye anaitwa Omar Abdalah Ramadhani ‘Mkereketwa wa Mwendokasi’ alisikika akisema “Magufuli kule aliko, aminia mzazi, Mungu akupe baraka zote mzazi, na asiyekupenda Mungu atamtokomeza, Watanzania tuko nyuma yako” kauli iliyomfanya Rais Magufuli amwite ili apige naye picha na baadaye kuombewa dua na kijana huyo.

Baada ya tukio hilo kufanyika na kurekodiwa, kijana huyo anaendelea kuwa maarufu katika mitandao ya kijamii huku baadhi ya watu wakimpachika jina la ‘Shabiki wa Mwendokasi’.
Tazama Video hapa

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post