Rais Magufuli : " Viongozi CHADEMA Msiwape Viroba Watoto wa Maskini na Kuwatanguliza Kwenye Maandamano...Tangulieni Nyie Mkione Cha Mtema Kuni"



Juzi Chama cha Demokrasia na maendeleo ‘CHADEMA’ kilitangaza mikakati mitatu ya kupinga ilichokiita ukandamizaji wa haki na demokrasia na kuitangaza siku ya September mosi mwaka kuwa ni siku ya maandamano nchi nzima.


Jana July 29 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alianza ziara ya siku nne katika mikoa ya Singida, Tabora, Shinyanga na Geita akitokea mkoani Dodoma, ambapo alizungumza na wananchi wa Manyoni Singida na kutoa onyo kwa watakaoanzisha maandamano.

"Wasije wakanijaribu mimi ni tofauti sana, na kama wapo watu wanawatumia wakawaeleze vizuri mimi sijaribiwi na wala sitajaribiwa, siasa nzuri wananchi wetu washibe, wapate madawa, nataka hao wanaotetea maandamano watangulie wao halafu wataona cha mtemakuni,wasiwatangulize watoto wa maskini,wao wanalala gesti,watoto wa maskini wanawapa viroba na kuwatanguliza...Vyama vyenyewe vimechokaa"- Alisema Rais Magufuli.


Hii hapa sauti ya Rais Magufuli  Msikilize.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527