Picha! Lowassa Akutana Uso Kwa Uso na Nape Nnauye Kwenye Msiba wa Mpiga Picha wa Tanzania Daima Joseph Senga


Aliyekuwa mgombea urais kupitia Chadema na Ukawa, Edward Lowassa amekutana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye leo katika jumuiko la kuuaga mwili wa aliyekuwa Mpiga picha wa Tanzania Daima, Joseph Senga.


Mwili wa Joseph Senga (58) umesafirishwa leo kwenda nyumbani kwao, Shushi-Nyambichi, Kwimba mkoani Mwanza kwa ajili ya mazishi hapo kesho. 




Akizungumza wakati wa kuuaga mwili wa marehemu Dar es Salaam mapema leo, msemaji wa familia, Charles Kapama amesema mazishi yatafanyika kesho saa nane mchana baada ya mwili kuwasili kijijini. 



Viongozi mbalimbali walijumuika na ndugu, jamaa na marafiki wa familia hiyo kuuaga mwili wa marehemu Senga ambaye alifariki dunia Julai 27 katika hispitali ya BLK, New Dehli India alikokwenda kupatiwa matibabu, katika uwanja wa mpira ulio jirani na nyumbani kwake, Sinza jijini Dar es salaam.



Viongozi hao ni pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika na Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea.



Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Joseph Senga, aliekuwa Mpiga Picha Mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima, aliefariki Dunia hivi karibuni, wakati wa shughuli ya kuaga mwili huo, iliyofanyika katika Uwanja wa TP, Sinza Uzuri, Jijini Dar es salaam.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Joseph Senga, aliekuwa Mpiga Picha Mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima, aliefariki Dunia hivi karibuni, wakati wa shughuli ya kuaga mwili huo, iliyofanyika katika Uwanja wa TP, Sinza Uzuri, Jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Joseph Senga, aliekuwa Mpiga Picha Mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima, aliefariki Dunia hivi karibuni, wakati wa shughuli ya kuaga mwili huo, iliyofanyika katika Uwanja wa TP, Sinza Uzuri, Jijini Dar es salaam.

Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Joseph Senga liwa katika Uwanja wa TP, Sinza Uzuri jijini Dar es salaam wakati wakiamuaga kwenda Kwimba, Mwanza kwa Maziko. Mwili wa Marehemu Joseph Senga unatarajiwa kuzikwa mara baada ya kufika.

Familia ya Marehemu Joseph Senga ikiwa ni yenye huzuni kubwa kuondokewa na Mpendwa wao.

Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Said Kubenea akizungumza.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe akizungumza.

Waziri Nape Nnauye akizungumza

Kushoto ni aliyekuwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja,Lowassa na Nape Nnauye
Waziri Nape Nnauye akiteta jambo na mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527