Picha! Kikao Cha Dharura Cha RCC Shinyanga,Makao Makuu ya Msalala ni NTOBO ,Isaka Sasa ni Mamlaka ya Mji



Jumatatu Julai 25,2016 kumefanyika kikao cha dharura cha Kamati ya Ushauri mkoa wa Shinyanga katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga ambacho kimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Shinyanga.

Kikao hicho kikiongozwa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack kilikuwa na ajenda mbili ambazo ni mapendekezo ya kuhamisha Makao Makuu ya Halmashauri ya Msalala kutoka kata ya Busangi kwenda kata ya Ntobo na mapendekezo ya kuanzisha mamlaka ya Mji Mdogo wa Isaka yaliyowasilishwa na mkurugenzi wa halmashauri hiyo Simon Berege.

Kikao hicho kimemaliza mvutano miongoni mwa madiwani wa halmashauri hiyo uliodumu kwa muda wa miaka mitatu kuhusu makao makuu ya halmashauri ya Msalala wilayani Kahama baada ya wajumbe wa kamati ya ushauri ya mkoa wa Shinyanga (RCC) kukubaliana kuwa makao makuu ya halmashauri hiyo yawe katika kata ya Ntobo kutoka kata ya Busangi.

Aidha kikao hicho kimeridhia maombi ya wananchi wa kata ya Isaka katika halmashauri ya Msalala kwamba kata ya Isaka yenye vijiji vine,vitongoji 18, kaya 3,373 na jumla ya watu 15,928 kuwa mamlaka ya Mji Mdogo.

Akiongoza kikao hicho mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack alisema msuguano miongoni mwa viongozi haina faida kwa wananchi haitakiwi kwani serikali inataka wananchi wake wapate maendeleo na makubaliano yaliyofikiwa sasa majengo yaanze kujengwa kuwasogezea wananchi huduma na kuhakikisha kuwa taratibu zinafuatwa katika kuiendeleza Mamlaka ya Mji wa Isaka.

Soma hapa chini mapendekezo ya kuhamisha Makao Makuu ya Halmashauri ya Msalala kutoka kata ya Busangi kwenda kata ya Ntobo yaliyowasilishwa na mkurugenzi wa halmashauri hiyo Simon Berege kwenye kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa wa Shinyanga kabla ya wajumbe wa kikao hicho kuridhia mapendekezo hayo leo Jumatatu,Julai 25 ,2016
Soma hapa chini mapendekezo ya kuanzisha Mamlaka ya Mji Mdogo wa Isaka yaliyowasilishwa na mkurugenzi wa halmashauri hiyo Simon Berege kwenye Kikao cha Kamati ya Ushauri ya mkoa wa Shinyanga kabla ya wajumbe wa kikao hicho kuridhia mapendekezo hayo leo Jumatatu,Julai 25 ,2016
Mwandishi wa Malunde1 blog ,Kadama Malunde ametuletea pia picha kutoka katika kikao hicho..Tazama hapa chini
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akiongoza kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa leo
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akizungumza ukumbini,kushoto kwake ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro 
Mkuu wa mkoa akizungumza.Wa kwanza kushoto ni naibe meya wa manispaa ya Shinyanga Grace Machiya


Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akiwa ukumbini
Viongozi wa mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini
Wakurugenzi wa halmashauri za wilaya wakiwa ukumbini
Kikao kinaendelea
Kikao kinaendelea
Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wakiwa ukumbini
Kikao kinaendelea
Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akizungumza katika kikao hicho
Mkurugenzi wa halmashauri ya Msalala Simon Berege akiwasilisha mapendekezo ya kuhamisha Makao Makuu ya Halmashauri ya Msalala kutoka kata ya Busangi kwenda kata ya Ntobo
Mkurugenzi wa halmashauri ya Msalala Simon Berege akiwasilisha mapendekezo ya kuanzisha Mamlaka ya Mji Mdogo wa Isaka 
Waandishi wa habari wakiwa ukumbini
Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wakiwa ukumbini
Wakuu wa wilaya za Kahama ,Fadhili Nkulu (kushoto) na Kishapu Nyabaganga Taraba wakiwa ukumbini
Kushoto ni mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna na mkurugenzi wa Kahama Mji Underson David Msumba (kulia)
Kushoto ni mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu Stephen Magoiga na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ushetu Matomora Michael (kulia)
Kikao kinaendelea
Wajumbe wa RCC wakiwa ukumbini

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akiteta jambo na katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela baada ya kufunga kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa wa Shinyanga.

Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post