Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Apiga "STOP" Ushoga,Utumiaji wa Shisha na Kuvuta Sigara Hadharani

 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amepiga marufuku vitu vitatu kutoonekana katika mkoa wa Dar es Salaam.


Akizungumza kwenye kongamano la Dini lililofanyika jana katika uwanja wa Taifa alisema..’Kwanza kwa watumiaji wa biashara ya Sheesha katika maeneo ya Bar, Clubs na sehemu zingine kuanzia jana ni marufuku katika maeneo hayo’- Paul Makonda

‘Pili ni marufuku kwa wavutaji wa Sigara kwenye sehemu za wazi kwani wataalamu wanasema ule moshi unamuathiri yule asiyetumia hiyo Sigara kuliko yule anayetumia Sigara’– Paul Makonda

‘Tatu ni marufuku kwa ushoga kwenye mkoa wangu wa Dar es Salaam na mashoga wote walio kwenye instagram na Facebook watakamatwa na wale wote wanao wa follow mashoga kwenye mitandao ya kijamii basi watakuwa na hatia ile kama ya mashoga‘- Paul Makonda

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post