Mgodi wa Buzwagi Wakabidhi Madawati 4494 Kwa Ajili ya Shule za Mkoa wa Shinyanga

Kampuni ya uchimbaji wa madini ya Acacia kupitia Mgodi wake wa Buzwagi umekabidhi madawati 4494 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 548 kwa ajili ya shule za sekondari na msingi za mkoa wa Shinyanga.Mwandishi wetu Kadama Malunde,anaripoti.



Akikabidhi madawati hayo,meneja mkuu wa mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo amesema Kampuni yake imekabidhi kiasi hicho cha madawati kwa lengo la kuunga mkono jitihada za mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Dkt. John Pombe Magufuli kupunguza uhaba wa madawati katika shule za msingi na sekondari.

“Mgodi wa Buzwagi unaunga mkono jitihada zinazofanywa na rais wa awamu ya tano,Dkt. John Pombe Magufuli katika kumaliza tatizo la wanafunzi kukaa chini,tumeamua kutekeleza kwa vitendo jitihada hizo” ,alieleza Mwaipopo.


Akipokea madawati hayo Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Bi Zainab Telack ameupongeza mgodi wa Buzwagi kwa mchango wao uliolenga kuunga mkono jitihada za mheshimiwa rais Magufuli, katika kuhakikisha kuwa watoto wote wanakaa kwenye madawati.


“Nimefarijika sana kuona mnaunga mkono serikali,tulikuwa na upungufu wa madawati lakini kwa msaada huu wa madawati mmesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo”,alisema Telack.


Aidha Mkuu huyo wa Mkoa wa Shinyanga amewataka wakurugenzi wa halmashauri zote katika mkoa wa Shinyanga kuwachukulia hatua kali za kisheria wazazi wote wanaowaachisha masomo wanafunzi.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Kahama Abeli Shija akishukuru kwa niaba ya halmashauri za mkoa wa Shinyanga, ameupongeza Mgodi wa Buzwagi kwa jitihada zao mbalimbali katika kutekeleza miradi ya kimaendeleo katika mkoa wa Shinyanga na hususani wilaya ya Kahama.


Hafla hiyo ya kukabidhi madawati ilifanyika Julai 28,2016 katika Shule ya Msingi Majengo iliyoko wilayani Kahama katika halmashauri ya mji wa Kahama ambapo ilihudhuriwa pia na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga,viongozi wa wilaya ya Kahama,uongozi wa Mgodi wa Buzwagi, walimu na wanafunzi wa shule ya msingi Majengo.

Meneja mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo(mwenye kofia ya bluu) akimpokea mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack wakati wa hafla ya kukabidhi madawati 4494 yaliyotolewa na Mgodi wa Buzwagi unaomilikiwa na Kampuni ya uchimbaji wa madini ya ACACIA.

Wanafunzi wa shule ya msingi Majengo iliyopo katika halmashauri ya mji wa Kahama wakipiga makofi kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wakati wa hafla ya kupokea madawati kutoka kwa uongozi wa Mgodi wa Buzwagi.
Wanafunzi wa shule ya msingi Majengo moja ya shule zilizonufaika na mchango wa madawati yaliyotolewa na Mgodi wa dhahabu wa Buzwagi.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi Zainab Telack wakifurahia jambo muda mfupi kabla ya makabidhiano.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama Simon Berege akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi madawati kutoka kwa Mgodi wa Buzwagi. 
Meneja mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo (kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telack wakati wa hafla ya kukabidhi madawati kwa uongozi wa mkoa wa Shinyanga.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Abel Shija akizungumza na kuushukuru Uongozi wa Mgodi wa Buzwagi unaomilikiwa na Kampuni ya Acacia kwa msaada wa madawati ambayo halmashauri ya mji wa Kahama itanufaika nayo.
Mhandisi Asa Mwaipopo Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi akizungumza wakati wa kukabidhi madawati yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 548 kwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga.

 Wanafunzi wakifuatilia hotuba ya meneja mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi Zainab Telack akikata utepe kuashiria kupokea madawati 4494 kutoka kwa uongozi wa Mgodi wa Buzwagi, anaekabidhi ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi Zainab Telack (katikati) akiwa amekaa na wanafunzi wa shule ya msingi majengo wakati wa hafla ya kupokea madawati kutoka kwa mgodi wa Buzwagi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi Zainab Telack (kulia) akiwa amekaa kwenye dawati na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Simon Berege akifurahia kukalia moja ya madawati yaliyokabidhiwa na Mgodi wa Buzwagi kwa Mkoa wa Shinyanga.


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi Zainab Telack akihutubia baada ya kupokea madawati 4494 kutoka Mgodi wa Buzwagi
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Shinyanga na wilaya ya Kahama wakiwa katika hafla hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkulu(katikati) akiteta jambo na katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela (kulia), mwingine katika picha ni mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama, Anderson Msumba (Kushoto).
Meneja mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo (Katikati) akiagana na Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Kahama Bwana Abel Shija, wengine katika picha kutoka kushoto kabisa ni Moses Msofe Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano ya Jamii, Mhandisi Richard Ojendo (wa pili kutoka kushoto) Mshauri wa Miradi Kampuni ya Acacia.

Wanafunzi wa shule ya Msingi Majengo wakifurahia mara baada ya shule yao kupokea baadhi ya madawati kutoka kwa uongozi wa Mgodi wa Buzwagi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527