Hii Hapa TOP 5 Ya Mastaa wa Soka Duniani Ambao ni Maarufu Sana Mitandaoni Kuliko Uwanjani

Mara nyingi imezoeleka wachezaji kupata umaarufu kutokana na kazi zao nzuri wanazofanya uwanjani na sio vinginevyo, Julai 19,2016,nimekutana na Top 5 ya mastaa wa soka ambao ni maarufu sana mitandaoni kuliko uwanjani.

5- Jack Wilshere twitter account yake inaonekana kuwa active kwa muda mwingi kiasi cha kufanikiwa kupata follower milioni 1.24, Wilshere akaunti yake mara nyingi anaweka picha zake za mazoezi, mechi, maisha binafsi na marafiki lakini zimeonekana kupata retweet nyingi kutoka kwa mashabiki wake.


Jack Wilshere

4- Mario Balotelli mshambuliaji wa kimataifa wa Italia ambaye kwa sasa amerudi katika klabu yake ya Liverpool akitokea AC Milan kwa mkopo ni mmoja kati ya wachezaji wanaotajwa kuwa maarufu katika mitandao ya kijamii kuliko uwanjani, kutokana na utovu wake wa nidhamu amekuwa na headlines nyingi binafsi mitandaoni kuliko headlines za uwanjani.


Mario Balotelli

3- Joey Barton ambaye kwa sasa hayupo katika Ligi Kuu England nae hatofautiani sana na Mario Balotelli, huyu nae ni maarufu mitandaoni kwa matukio ya kizembe na utukutu uwanjani, kitu ambacho kimekuwa kikimfanya ajadiliwe mara kwa mara mitandaoni kwa upande hasi kuliko kujadiliwa kwa mambo mazuri.


Joey Barton

2- Emmanuel Adebayor amewahi kucheza baadhi ya vilabu vikubwa barani Ulaya kama Arsenal, Man City, Real Madrid na Tottenham Hotspur, anatajwa kama mmoja kati ya mastaa ambao wanapenda kutumia facebook na twitter na ukilinganisha na matatizo yake na familia yake yaliokuwa yakijadiliwa kupitia facebook kilimfanya awe maarufu zaidi mtandaoni.


Emmanuel Adebayor

1- Mchezaji wa kimataifa wa Ghana ambaye anaichezea klabu ya FC UFA ya Urusi Emmanuel Frimpong amekuwa maarufu kwa sababu ya kuwa active sana twitter na kuwa na rekodi ya kutweet 8k tweets, rekodi ambayo ni zaidi ya muda wake alioonekana uwanjani, yaani ameonekana mtandaoni mara nyingi zaidi kuliko uwanjani.


Emmanuel Frimpong

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post