Leo Juni 5, ni Siku ya Mazingira Duniani.
Akizungumza wakati wa zoezi la usafi kijijini hapo Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Ilogi Christopher Galila amesema hatua ya wafanyakazi kusafisha mazingira ya kijiji ni funzo muhimu kwa wananchi wengine na kusema kwamba uchafuzi wa mazingira hautavumiliwa katika maeneo yoyote kijijini humo.
“Pamoja na kutusaidia kusafisha hii leo meneo mbalimbali kwenye vizimba vya uchafu ambavyo baadhi vimekuwa na taka kwa muda mrefu pamoja na soko letu, Mgodi umetupatia mapipa kumi na tano ya kutupia taka ambayo yatatusaidia katika siku za usafi za kila juma, kwani kijiji chetu kina utaratibu wa kukusanya na kukagua usafi wa mazingira kila siku ya Jumamosi.”
Naye Kaimu Meneja wa Ufanisi wa Mgodi wa Bulyanhulu Bwana Onesmo Kabeho amesema timu ya wafanyakazi imefurahi mwitikio wa wananchi walioungana na wafanyakazi kusafisha mitaa, mitaro, vizimba vya taka na soko la kijiji.
“Sisi leo tumefurahi sana kung’arisha maeneo mbalimbali kijijini hapa kwa kuondoa kero ya uchafu ambao ni hatari kwa mazingira, tunatoa mwito kwa wanajamii wote kutunza mazingira kwa njia mbalimbali ikiwemo kudhibiti takataka hasa plastic ili watoto wetu na vizazi vijavyo visipate athari ya uchafuzi wa mazingira wa sasa”.
Social Plugin