Picha 85!! Mwenyekiti wa CCM Awafuturisha Waislamu Mkoa Wa Shinyanga,Sheikh Mkuu Apongeza,Askofu Atoa Neno Kwa Magufuli


Juni 29,2016 kumefanyika tukio muhimu mjini Shinyanga ambapo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga ndugu Erasto Kwilasa (pichani) amewaandalia chakula cha pamoja “futari” waumini wa dini ya kiislamu mkoa wa Shinyanga ikiwa ni sehemu ya kuutukuza mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Tukio hilo limefanyika leo jioni/usiku kuanzia katika Ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na waumini na viongozi wa dini ya kiislamu wakiongozwa na Sheikh Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ismail Habibu Makusanya.

Wengine waliohudhuria ni viongozi wa vyama vya siasa na serikali,viongozi wa madhehebu mengine ya dini wakiongozwa na Askofu wa Kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga, Askofu Dr. John Nkola na watu mbalimbali wenye mapenzi mema.

Akizungumza wakati wa kula chakula hicho "futari" mwandaaji wa futari hiyo ambaye ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Erasto Kwilasa aliwashukuru waumini wa dini ya kiislamu kukubali kushiriki katika futuru hiyo na kudai kuwa ameamua kufanya hivyo ili kuonesha kwa vitendo kuwa anawapenda watu wa Shinyanga bila kujali makabila,dini wala rangi zao.

“Nawashukuruni sana ndugu zangu tumekusanyika sote hapa,tupo hapa kushirikiana pamoja kwa kupata futari ya pamoja,mimi binafsi naamini katika ibada hii tutakuwa tumetenda jambo jema mbele ya mwenyezi mungu hasa katika kutekeleza nguzo muhimu miongoni mwa nguzo tano za kiislamu,funga ya mwezi mtukufu ambayo ni nguzo ya nne”,alisema Kwilasa.

“Ndugu zangu mlikuwa na nafasi ya kutoa udhuru kwamba mimi niliyewaalikeni kuwa ni kiongozi wa chama,lakini kwa upendo mlionionesha leo hii mmedhihirisha ule usemi wa kuwa serikali na chama havina dini bali wanachama wake wana dini zao na hii ndiyo maana mmekuja kwa wingi na mpaka sasa tupo pamoja hapa bila ubaguzi wa aina yoyote”,aliongeza Kwilasa.

Kwilasa alitumia fursa hiyo kuwataka wanasiasa kuacha kubaguana kwani binadamu wote ni wa mwenyezi mungu huku akimuomba mungu kupokea funga za waumini wote wa mkoa wa Shinyanga na taifa kwa ujumla.

“Kwa kutambua kazi nzuri zinazofanywa na rais John Pombe Magufuli na timu yake yote,naomba tuendelee kumuombea sana kwa mungu ili aweze kufanikisha malengo yake aliyowaahidi wananchi”,alisema Kwilasa.

Katika hatua nyingine Kwilasa aliwaomba viongozi wote wa madhehebu ya dini kusaidiana na viongozi wa serikali mkoa wa Shinyanga kupiga vita vitendo vya mauaji dhidi ya vikongwe,ubakaji na ulawiti kwa watoto,utumiaji wa madawa ya kulevya na ukatili wa kijinsia.

Kwa upande wake Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sheikh Ismail Habibu Makusanya alimpongeza mwenyekiti huyo wa CCM kuandaa chakula cha pamoja kwa ajili ya waumini wa dini ya kiislamu na kusema kuwa kitendo alichokifanya kina dhawabu kubwa kwa mwenyezi mungu.

“Ukimuona mja anashughulika kuwalisha watu, wa kweli na wasio wakweli,wacha mungu na wasio wacha mungu huyu ameshika kazi ya mungu..sasa mwenyeji wetu ulichokifanya hapa sisi hatuwezi kukulipa lakini hiki ulichofanya ni kafara kubwa sana katika maisha yako ,ni hifadhi kubwa sana katika maisha yako,ni sadaka kubwa sana,kuwaita na kuwalisha waliofunga ni kazi kubwa,mungu akuzidishie pale ulipotoa”,aliongeza Sheikh Makusanya.

Naye Askofu wa Kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga, Askofu Dr. John Nkola alisema ni mara kwanza yake ya kwanza kukaribishwa kwenye futari kubwa kama hiyo na kuwashukuru waislamu kukusanyika pamoja kushiriki pamoja kwa futari na kwamba mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ni kwa ajili ya utukufu wa mungu.

Askofu Nkola alitumia fursa hiyo kuwataka watanzania kujenga mshikamano na umoja uliopo kwani umoja wa madhehebu ya dini ndiyo uzima na amani ya taifa la Tanzania.


“Tukishikamana na kumhubiri mwenyezi mungu ambaye ni wa amani,nchi yetu itaendelea kuwa na amani sana,tuendelee kushikamana,na tuendelee kumuombea rais Magufuli anafanya mambo makubwa ambayo siyo kila mtanzania atayapenda hata kidogo”,alisema Askofu Nkola


“Sasa sisi kazi yetu siyo siasa lakini maandiko na misahafu inatuagiza kuwaombea wale ambao mwenyezi mungu amewapa madaraka ya kutawala,tumuombee sana rais wetu,pamoja na serikali yetu na nchi yote kwa ujumla tuendelee kutulia kwa amani,tuendelee kuwa kimbilio la wanyonge wanaonyanyaswa katika nchi zao”,aliongeza askofu Nkola.

Malunde1 blog huwa haipitwi na matukio,Mwandishi mkuu wa mtandao huu,Kadama Malunde alikuwepo eneo la tukio,ametusogezea picha 85..Shuhudia mwenyewe hapa chini

Wa kwanza kushoto ni Askofu wa Kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga, Askofu Dr. John Nkola,wa kwanza kulia ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sheikh Ismail Habibu Makusanya wakiwa katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga usiku huu

Wa pili kutoka kushoto ni mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulah Hafeez Mukadam akiwa na viongozi wa dini ya kiislam mkoa wa Shinyanga

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga ambaye ndiye mwandaaji wa Futari hiyo ndugu Erasto Kwilasa akizungumza ukumbini na kuwashukuru waumini wa dini ya kiislamu kwa kujitokeza kwa wingi kufuturu kwa pamoja
Mwenyekiti huyo wa CCM mkoa wa Shinyanga ndugu Erasto Kwilasa alisema wamekusanyika hapo kwa ajili ya kuutukuza mwezi mtukufu wa Ramadhani

Tunamsikiliza Kwilasa.....
Kwilasa alisema ameandaa futari hiyo ikiwa ni ishara ya kuonesha ushirikiano kwa vitendo ikiwa ni mambo aliyousiwa na wazee wa mji wa Shinyanga alipokutana nao na kufanya mazungumzo kwamba miongoni mwa usia wao mkubwa ni kujitahidi kuwa karibu na watu.

Meza kuu wakitafakari...

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga akitoa hotuba fupi

Tunafuatilia hotuba.....
Kwilasa akizungumza ukumbini ambapo aliwahakikishia wakazi wa Shinyanga kuwa atafanya kazi na kila kundi katika jamii kwa nguvu na bidii zake zote
Askofu wa Kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga, Askofu Dr. John Nkola akizungumza ukumbini ambapo aliwasihi watanzania kudumisha mshikamano walio nao ili kuhakikisha kuwa amani ya nchi haitoweki
Askofu wa Kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga, Askofu Dr. John Nkola akisisitiza umoja na mshikamano miongoni mwa watanzania bila kujali dini,makabila wala rangi zao.

Askofu John Nkola akifurahia jambo...
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sheikh Ismail Habibu Makusanya akitoa shukrani za mualiko wa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga kushiriki futari ya pamoja ambapo alisema hilo ni jambo jema linalofurahiwa sana na mwenyezi mungu

Meza kuu wakimsikiliza Sheikh Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya

Sheikh Makusanya akizungumza ukumbini
Tunamsikiliza Sheikh wa mkoa wa Shinyanga

Sheikh Makusanya alimpongeza Kwilasa kwa kuona umuhimu wa kuwakaribisha chakula waislamu waliofunga huku akiwahamasisha wanadamu kuwa na moyo wa kujitolea ili kupata dhawabu kutoka kwa mwenyezi mungu

Wa pili kutoka kulia ni mkuu wa polisi wilaya ya Shinyanga Richard Ngede
Sheikh Makusanya akizungumza ukumbini ambapo pia alihamasisha watanzania kuendelea kushikamana ili kudumisha amani ya nchi

Meza kuu wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea...Wa kwanza kulia ni mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Kaanali mstaafu Tajiri Maulid
Waumini wa dini ya Kiislamu wakiwa ukumbini

Waumini wa dini ya kiislamu na wageni waalikwa,katikati ni Diwani wa Kata ya Kambarage katika manispaa ya Shinyanga Hassan Mwendapole
Washiriki wa tukio hilo wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini
Tunafuturu pamoja.....


Washiriki wakiwa ukumbini

Tunafuatilia kinachoendelea ukumbini

Akina mama wakiwa ukumbini

Tunakunywa uji....

Viongozi wa CCM na dini ya kiislam wakiwa meza kuu,wa kwanza kushoto ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Erasto Kwilasa

Tunakula pamoja

Tunafuturu pamoja

Viongozi wa madhehebu ya dini,serikali na dini ya kiislamu wakiwa meza kuu huku washiriki wengine wakiwa katika mstari kwa ajili ya chakula

Meza kuu wakila chakula

Zoezi la kuchukua chakula linaendelea.

Tunachukua chakula

Zoezi la kuchukua chakula linaendelea

Tunakula chakula......

Meza kuu wakiendelea kula chakula

Tunakula...

Akina mama wakila chakula

Tunakula...


Akina mama wakiwa ukumbini








Tunakula.....

Hapa ni kula tu....

Tunafuturu...


Tunaendelea kula...




Tunaendelea kula...








Tunakula.....

Akina mama wakiendelea kula ukumbini






Kila mmoja alikula....

Baada ya kumaliza kula...



Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Erasto Kwilasa akikumbatiana na Sheikh Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Ismail Habibu Makusanya

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Erasto Kwilasa akikumbatiana na Askofu John Nkola

Hongera sana kwa kuandaa futari ndugu Kwilasa.....

Askofu John Nkola na Kaanali Mstaafu Tajiri Maulid wakiondoka ukumbini baada ya kufuturu

Hongera kwa kazi nzuri....

Mweka hazina wa CCM mkoa wa Shinyanga bwana Mapalala akiwa na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga baada ya shughuli kumalizika.

Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527