Mwenyekiti wa CHADEMA Atekwa,Ateswa na Kutelekezwa Porini Huko Simiyu

Natalis Mataba(62)-Picha kutoka Maktaba yetu
Mmoja wa maafisa usalama wa Taifa wilayani Maswa mkoani Simiyu, anadaiwa kumteka, Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kata ya Sola wilayani humo Natalis Mataba(62) kisha kumpiga, kumtesa na kumtelekeza porini katika wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza.

Tukio hilo linadaiwa kutokea juzi majira ya saa 2:30 asubuhi.Akizungumza na Waandishi wa habari akiwa hospitali ya serikali ya wilaya ya Maswa akipatiwa matibabu, Mataba amesema kuwa afisa huyo alifika nyumbani kwake majira ya saa 2:30 asubuhi akiwa ameambatana na mlinzi wa ofisi hiyo na kumtaka waongozane naye ofisini kwao.
Chanzo-Simiyunews Blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post