Mbunge Auawa Kwa Kupigwa Risasi na Kuchomwa Kisu Akiwa Kwenye MkutanoMbunge wa chama cha Leba nchini Ungereza Jo Cox ameaga dunia baada ya kupigwa risasi na kuchomwa kisu akiwa kwenye mkutano katika eneo lake la ubunge kaskazini mwa Uingereza.


Cox Ndiye mbunge wa kwanza kuuawa nchini Uingereza tangu Ian Gow auawe mwaka 1990.

Mwanamme mmoja mwenye umri wa miaka 52 aliyetajwa na majirani kama mtu asiye na marafiki amekamatwa na silaha kupatikana.


Walioshuhudia wanasema kuwa mbunge huyo aliingilia kati mzozo kati ya wanaume wawili eneo ambapo alikuwa akikutana na watu eneo lake la ubunge.

Mtu mmoja aliyeshuhudia alisema risasi ilifyatuliwa wakati Bi Cox aliingilia kati.

Kisha muuaji akaanza kumchoma kisu alipokuwa amelala chini.
Chanzo-BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post