Maandalizi ya Mahakama ya Mafisadi Yaanza

Wakati Bunge likiwa limepitisha sheria ya uanzishwaji wa Mahakama ya Mafisadi nchini, Jukwaa la Haki Jinai ambalo linajumuisha Taasisi za umma na serikali limekutana kujipanga namna zitakavyoweza kufanya kazi kwa ufanisi kwenye Mahakama hiyo.


Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, mara baada ya kufungua kikao hicho cha kazi cha siku mbili cha jukwaa hilo.


Dk. Mwakyembe alisema jukwaa hilo limehudhuriwa na viongozi wote wa Taasisi ambazo zipo kwenye mfumo wa haki jinai ikiwemo Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa, Mahakama, Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa(Takukuru).


Alisema kikao hicho kinafanyika kipindi muafaka kwa sababu jana Bunge lilipitisha muswada wa marekebisho ya sheria mbalimbali ambao unatoa mwanya wa kuanzisha mahakama ya mafisadi na makosa ya rushwa.


Alibainisha vyombo hivyo vinaangalia jinsi gani kimoja kimoja kwa ushirikiano vitakavyoweza kufanikisha uanzishaji wa Mahakama hiyo.


Kikao hicho kilihudhuriwa na idara ya polisi ambayo inatakiwa ipeleleze haraka, Takukuru ifanye uchunguzi kwa haraka, Timu ya DPP na waendesha mashtaka wake wote ifanye kazi kwa ufanisi sana kesi zisikae, Mahakama nayo kama kuna vitu vinakwamisha vitatuliwe.


Alisema chombo hicho kinatafakari namna vyombo hivyo vitakavyoshirikiana ili mahakama hiyo iweze kufanya kazi kwa ufanisi kama Rais alivyoahidi.

Hata hivyo alisema pamoja na hilo wanajadili changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika usimamiaji wa haki jinai nchini.


Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mashtaka nchini,Buswalo Mganga alisema changamoto zinazoikabili haki jinai nchini ni uhalifu ambao unafanywa na watanzania wenyewe na miongoni mwao wengine wanatoka nje na washirikiana na watanzania na vyombo vya habari.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527