Hawa Ndiyo Mastaa Watabeba Jeneza la Bondia Muhammad Ali Wakati wa Mazishi

Bado dunia na mashabiki wa mchezo wa Boxing wapo katika maombolezo ya msiba wa bondia mahiri aliyewahi kushinda mikanda mbalimbali ya Boxing Duniani Muhammad Ali, leo Juni 7 2016 mitandao mbalimbali imeripoti baadhi ya mastaa watakaobeba jeneza la Muhammad Ali.


Kutoka kushoto ni Lennox Lewis alipokabidhiwa tuzo yake ya mwanamichezo bora wa mwaka wa BBC na Muhammad Ali alipopewa tuzo ya heshima ya mwanamichezo bora wa karne 1999

Bondia wa zamani wa uzito wa juu Lennox Lewis ambaye amewahi kushinda mwanamichezo bora wa mwaka BBC 1999 pamoja na Muhammad Ali aliyepewa tuzo ya mwamichezo bora wa karne, ametajwa kuwa miongoni mwa mastaa watakaobeba jeneza la Muhammad Ali.


Kutoka kushoto ni Muhammad Ali enzi za uhai wake na Will Smith

Msanii Will Smith ni moja kati ya mastaa waliotajwa kupewa nafasi ya kubeba jeneza la Muhammad Ali. Muhammad Ali alifariki Ijumaa iliyopita katika hospitali ya Phoenix Arizona akiwa na umri wa miaka 74, lakini taarifa zinaeleza kuwa atazikwa nyumbani kwao Louisville Kentucky.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post