Mbunge wa Shinyanga Mjini Stephen Masele Ang'aka Soko Kuu Kuwa Chafu,Afanya Pia Ziara Kiwanda Cha Jambo na Shule ya Msingi Bugweto,Picha ziko Hapa


Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Steven Masele akionyesha sura ya kuchukizwa na uchafu ambao umekithiri kwenye Soko kuu la Mji wa Shinyanga. Kulia ni mmoja wa wafanyabiashara katika soko hilo akielezea changamoto ya uchafu katika soko hilo hali inayosababisha wakose wateja.********

Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini Mheshimiwa Stephen Masele amemuagiza Ofisa afya wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Kheri Nakuzerwa kuhakikisha anasimamia kikamilifu usafi wa soko kuu hadi pale ujenzi wa ghuba la kuhifadhi uchafu litakapokamilika.


Mheshimiwa Masele ametoa agizo hilo leo alipofanya ziara yake katika Soko hilo na kukuta limekithiri kwa uchafu hadi milangoni, hali iliyomfanya amuagize Ofisa afya huyo kuhakikisha soko hilo linakuwa safi muda wote ili kuepuka mji kutokea magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindu pindu.


Akizungumza ndani ya Soko hilo Masele amesema haiwezekani sehemu ya kuuzia bidhaa ya chakula inakuwa katika hali ya uchafu huku uongozi wa halmashauri ukiangalia jambo hilo ambalo ni hatari kwa afya ya binadamu wakiwamo wateja pamoja na wafanyabiashara, na hivyo kumuagiza Ofisa afya huyo kuliweka soko hilo katika hali ya usafi.

“Yaani uchafu unarundikana hadi mlangoni na wewe Ofisa afya unaridhika na hali hii eti kisa unasingizia ghuba la uchafu bado halijakamilika kujengwa? Ina maana hauna njia nyingine ya kuchukua uchafu huu na kuupeleka mahali panapostahili na wakati hapo halmashauri kuna magari ya kubebea uchafu yamejaa”,alieleza Masele.


"Hivyo nakupa Masaa 24 Soko hili liwe katika hali ya usafi tofauti na hapo hatutaelewana, Soko likiwa chafu wateja hawezi kuja kununua Chakula humu, na mwisho wa siku Serikali ina kosa kukusanya ushuru kama inavyotakiwa na hivyo kudidimiza uchumi wa halmashauri na kukosa pesa za miradi ya maendeleo",aliongeza Masele.


Naye afisa afya wa Manispaa ya Shinyanga Kheri Nakuzerwa amekiri soko hilo kuwa chafu kutokana na ujezi wa ghuba la kuhifadhia taka ngumu kuendelea kujengwa sokoni hapo, na kuahidi kuondoa taka zilizokithiri ndani ya soko pamoja na kutafuta mbinu za kuhifadhi uchafu hadi pale ujenzi wa ghuba utakapokamilika ndani ya wiki mbili.


Mbali na kutembelea soko hilo pia mheshimiwa Masele ametembelea kiwanda cha Jambo pamoja na Shule ya Msingi Bugweto iliyopo kata ya Ibadakuli ambayo ina kabiliwa na changamoto lukuki ikiwamo ubovu wa majengo na uhaba wa madawati.

Mwandishi wetu Marco Maduhu alikuwep katika ziara zote tatu,ametuletea picha kuanzia mwanzo mpaka mwisho...Angalia picha hapa chini


ZIARA SOKO KUU-Mfanyabiashara wa Soko hilo Lydia Shilema akimuelezea Mbunge Masele jinsi gani soko hilo lilivyokosa umaarufu kwa kukithiri kwa uchafu pamoja na miondombinu yake kuwa mibovu na kuzidiwa na soko la Nguzo Nane ambapo wafanyabiashara wengi wameanza kukimbilia huko.
Uchafu uliopo kwenye lango kuu la kuingia ndani ya soko hilo
 
Wa kwanza Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akionyesha sura ya kuchukizwa na uchafua ambao umekithiri kwenye Soko kuu la Mji wa Shinyanga na kumuagiza Ofisa afya wa Halmshauri ya Manispaa ya Shinyanga Kheri Nakuzerwa kulia kwake mwenye Miwani kusimamia usafi wa soko hilo kuwa safi muda wote.

Mheshimiwa Masele akisalimiana na mfanyabiashara katika soko hilo
Mheshimiwa Masele akitoa maelekezo kwa wafanyabishara wa soko hilo na kuwaomba wakae kwenye vikao vyao na kuafikiana wapi wataenda kujihifadhi kwa muda kufanya biashara zao ili kupisha ukarabati wa soko hilo kuanza kujengwa na kuwa la kisasa.

Mheshimiwa Masele akimpatia maagizo afisa Afya Kheri Nakuzerwa hadi kufikia masaa 24 Soko hilo liwe katika hali ya usafi

Mheshimiwa Masele akisalimiana na wafanyabiashara wa soko hilo


ZIARA KIWANDACHA JAMBO-Mheshimiwa Masele (kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Jambo kinachotengeneza soda kilichopo Mjini Shinyanga Salumu Hamisi Mbuzi wakielekea kuangalia namna uzalishaji wa bidhaa kwenye kiwanda hicho unavyofanyika.

Mheshimiwa Masele (kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Jambo kilichopo Mjini Shinyanga Salumu Hamisi Mbuzi wakielekea kuangalia namna uzalishaji wa bidhaa kama vile maji na soda ndani ya kiwanda hicho unavyofanyika

Mheshimiwa Masele akiwa ndani ya kiwanda cha Jambo kinachozalisha soda na maji


Kushoto ni Mkurugenzi wa Kiwanda  cha Jambo Salum Hamisi Mbuzi akitoa maelezo ya uzalishaji wa kiwanda hicho jinsi kinavyofanya kazi hadi kupeleka bidhaa Sokoni.


Mkurugenzi wa Kiwanda hicho cha Jambo Salum Hamisi Mbuzi akitoa maelezo ya uzalishaji wa kiwanda hicho jinsi kinavyofanya kazi hadi kupeleka bidhaa Sokoni.
 
Mfanyakazi wa kiwanda cha jambo akitoa maelezo namna wanavyofanya kazi 
Uzalishaji wa soda ukiendelea

Soda zikiwa tayari
Mheshimiwa Masele akizungumza jambo

Mbunge Steven Masele akimpongeza mkurugenzi wa kiwanda hicho Salumu Hamisi Mbuzi ambaye ni muwekezaji mzawa kuweka kiwanda chake katika mji wa Shinyanga ambapo umepunguza Ukosefu wa ajira kwa vijana ikiwa kiwanda hicho kimeajiri vijana zaidi ya 250.
Mkurugenzi wa kiwanda cha Jambo Salum Hamisi Mbuzi akieleza namna wanavyofanya uzalishaji
Mkurugenzi wa kiwanda cha Jambo Salum Hamisi Mbuzi akiwa na mbunge Masele na wafanyakazi wa kiwanda hicho

Wafanyakazi wa kiwanda cha jambo wakiendelea na kazi
Ndani ya kiwanda soda zikiwa tayari
Mheshimiwa Masele akiwa kiwandani
Mheshimiwa Masele akiwa na Salum hamis Mbuzi wakiteta jambo wakati wa ziara hiyo
Mheshimiwa Masele akisikiliza maelezo namna mitambo inavyofanya kazi katika kiwanda hicho
ZIARA SHULE YA MSINGI BUGWETO-Wanafunzi wa Shule ya Msingi Bugweto wakifurahia kumuona Mbunge wao Stephen Masele pamoja na diwani wa viti maalum tarafa ya Ibadakuli mheshimiwa Zuhura Waziri wakiamini kuwa kilio chao cha ubovu wa majengo na uhaba wa madawati ndiyo utakuwa mwisho.

Mheshimiwa Masele akiwa na diwani wa viti maalum tarafa ya Ibadakuli mheshimiwa Zuhura Waziri wakisalimiana na wanafunzi wa shule ya msingi Bugweto


Miundo mbinu ya shule hiyo ikionekana mibovu huku ukuta zikiwa zimetokeza nyufa na wanafunzi wakisoma chini ya Vumbi.

Moja ya madarasa katika shule hiyo

Mheshimiwa Masele akiongea na wanafunzi wa shule hiyo na kuwaahidi kutoa shilingi Milioni 1.5 kwa ajiri ya kukarabati majengo ya shule hiyo na kuwekewa sakafu na kuzibwa nyufa zake ili wasome katika mazingira mazuri

Mheshimiwa Masele akiwa na wanafunzi

Mheshimiwa Masele akifurahia jambo na wanafunzi


Kushoto ni diwani wa viti maalum tarafa ya Ibadakuli mheshimiwa Zuhura Waziri akizungumza na baadhi ya walimu wa shule hiyo,wa pili kulia ni mheshimiwa Stephen Masele
Picha ya pamoja -Mheshimiwa Masele,diwani wa viti maalum tarafa ya Ibadakuli( wa pili kulia mwenye nguo ya njano na ushungi) mheshimiwa Zuhura Waziri na walimu wa shule hiyo

Picha zote na Marco Maduhu-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post