Waziri Nape Nnauye Akutana na Wadau Wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mkoa wa ShinyangaWaziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye amekutana na wadau wa habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo mkoani Shinyanga jana Aprili 15,2016 katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga.
 
Akizungumza na wadau hao baada ya kusikiliza michango ya wadau hao zikiwemo kero zinazowakabili,alisema wizara yake imedhamiria kuleta mapinduzi ya kweli katika maeneo hayo manne katika wizara hiyo.

Alisema hivi sasa anazunguka katika mikoa mbalimbali nchini na kukutana na wadau wa wizara yake kwani lengo ni kutaka kuipeleka wizara hiyo kutoka Dar es salaama kwenda mikoani kwani ndiko kuna wadau wengi.
 
"Ninaendelea na ziara yangu kukutana na wadau wa sekta hizi nne,tunataka sekta hizi ziguse kila mahali hapa nchini,tunataka maendeleo makubwa katika tasnia ya habari,michezo,sanaa na utamadani",alisema Nnauye.
Kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Josephine Matiro ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga akizungumza katika mkutano huoWadau wa habari,michezo,sanaa na utamaduni wakiwa ukumbini


Mkutano unaendelea

Wadau wa habari,michezo,sanaa na utamaduni wakiwa ukumbini

Wadau wakiwa ukumbini

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post