Wananchi Watatu Washikiliwa Polisi kwa Kusafirisha Wahamiaji Haramu


Wakazi wawili wa jijini Dar es Salaam na mmoja wa mkoani Iringa, wanashikiliwa na Polisi mkoani Tanga kwa tuhuma za kuingiza na kusafirisha wahamiaji haramu 10 kutoka nchini Ethiopia.Watuhumiwa hao ni Ali Juma (24) ambaye ni dereva wa gari namba T 113 DCV aina ya Toyota Hiace iliyokuwa ikisafirisha watu hao na Joseph John (42), wote wakazi wa Dar es Salaam. Mwingine ni Idi Juma (38), mkazi wa Iringa.


Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Tanga, Leonard Paul alisema watuhumiwa wote walikamatwa saa 8:00 usiku wa kuamkia Aprili 14 mwaka huu, katika eneo la Misajini wakati gari hilo likiendelea na safari.


“Misajini iko katika barabara kuu ya Hedaru - Mombo ambapo baada ya askari wetu kupata taarifa za wasafiri hao, waliwafuatilia na kuwakamata,” alisema.


Alisema, kumekuwa na matukio ya mara kwa mara ya kukamatwa kwa wahamiaji haramu mkoani kwetu lakini chanzo chake pamoja na mambo mengine ni jiografia ya mkoa yenye njia nyingi za panya.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post