Vipaza Sauti Vya Bunge Vyaharibika, Bunge Lasimama kwa Dakika 36

Shughuli za Bunge la Muungano leo zilisimama kwa dakika 36 kabla ya kuendelea tena, baada ya vipasa sauti vya ukumbini kushindwa kufanya kazi.

Spika wa Bunge, Job Ndugai amelazimika kuahirisha shughuli mara baada ya kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu ambacho hata hivyo wabunge walichukua muda mrefu kuuliza maswali kutokana na kuhama hama wakitafuta mahali pa kusikika.

Awali, wabunge waliokuwa na nafasi ya kuuliza maswali walilazimka kuhama maeneo yao na kuzua minong’ono ndani ya ukumbi, huku Mbunge wa Mkuranga (CCM), Abdallah Ulega na Mbunge wa Manonga (CCM), Seif Gulamali wakilazimika kuuliza maswali yao wakiwa uso kwa uso na Waziri Mkuu mbele ya ukumbi.

Hata hivyo, kuna hali ya sintofahamu, kwani vipaza sauti vimeharibika ikiwa ukumbi huo umefanya kazi kwa siku sita tu tangu ulipokabidhiwa baada ya ukarabati mkubwa.

April 18, Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson alikabidhiwa ukumbi huo ikielezwa kuwa ulikuwa umefanyiwa matengenezo makubwa katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kuuboresha.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527