RAIS SHEIN AMTEUA HAMAD RASHID WA ADC KUWA MJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI


Rais wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua mwenyekiti wa chama cha ADC Hamad Rashid Mohamed kuwa mjumbe wa Baraza la wawakilishi.


Uteuzi huo wa Rais Dkt Shein umefuata baada ya leo kutoa hotuba na kuzindua Baraza la wawakilishi ambapo pamoja na mambo mengine amesisitiza umoja na mshikamano miongoni mwa wananchi.

Wengine walioteuliwa kuwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ni pamoja na  1.Mohamed aboud Mohamed 2. Amina Salum Ali  3. Moulin Castico 4. Balozi Ali karume  5. Said Soud Said na 6. Juma Ali Khatibu

Aidha uteuzi huo umeanza hii leo tarehe 05.04.2016.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post