HII HAPA TAARIFA YA TAKUKURU KUHUSU VIGOGO WA TRA NA EGMA KUFIKISHWA MAHAKAMANI







TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) leo tarehe 1/4/2016 imewafikisha Mahakamani aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania na Mwenyekiti wa ‘Enterprise Growth Market Advisors Ltd’ (EGMA), Bw. Harry Msamire Kitilya; aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Ushirikiano na Uwekezaji wa Benki ya Stanbic Tanzania, Shose Mori Sinare pamoja na Aliyekuwa Mwanasheria wa Benki ya Stanbic Tanzania, Bw. Sioi Graham Solomon.


Washtakiwa wote wanashtakiwa kwa makosa ya:- Kula njama na kujipatia kwa udanganyifu kinyume na kifungu Na. 384 cha Kanuni ya Adhabu (Cap 16 R.E. 2002) ; Kughushi kinyume na kifungu Na. 333,335 (a) na 337 cha Kanuni ya Adhabu (Cap 16 R.E 2002) ; Utakatishaji wa fedha haramu kinyume na kifungu Na. 12 (a) 13 (a) cha Sheria ya ya Utakatishaji fedha Na. 12 ya Mwaka 2006 ‘Anti- Money Laundering Act’.


Mashtaka hayo yalisomwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Mhe. Hakimu Emirius Mchauro. Kwa upande wa Jamhuri kesi hii inasimamiwa na Mwendesha Mashtaka Mwandamizi wa Serikali Herman Tibabyekomia, Christopher Msigwa na Mwendesha Mastaka wa TAKUKURU Stanley Luoga. Washtakiwa wanatetewa na Wakili wa Kujitegemea Ringo Tenga, Rosai Mbwambo, Semo na Nyaisa.


Washitakiwa wote watatu wamepelekwa rumande, wamekosa dhamana kwani Kifungu Na. 148 (5) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) Kinazuia utoaji wa dhamana kwa washtakiwa wa Utakatishaji wa fedha haramu. Kesi hii itatajwa tena tarehe 8/4/2016.


IMETOLEWA NA
OFISI YA AFISA UHUSIANO
TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA, MAKAO MAKUU
1 APRIL, 2016.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527