ANGALIA PICHA- POLISI WAKITEKETEZA KWA MOTO MASHAMBA YA BANGI HUKO SIMIYU



Jeshi la Polisi Mkoani Simiyu limefanikiwa kuharibu zaidi ya hekari tatu za mashamba yaliyokuwa yamelimwa zao haramu la bangi, katika vijiji vya Ihusi kata ya Ihusi pamoja na Mwasinasi kata ya Matondo katika wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu.

Mbali na kuharibu mashamba hayo jeshi hilo lilifanikiwa kukamata bangi zaidi ya tani tatu, ambazo tayari zilikuwa zimevunwa na wananchi waliokuwa wakijihusisha na kilimo hicho.

Hata hivyo katika hali isiyokuwa ya kawaida baada ya wananchi wa vijiji hicho kuona askari wakiingia kwa msafara mkubwa wa magari, wengi walikimbia na kuacha nyumba pamoja na watoto ili kukwepa mkono wa sheria.

Licha ya baadhi ya familia kukimbia, jeshi hilo lilikamata baadhi ya watuhumiwa ambao walieleza kuficha bangi ikiwa pamoja na kumiliki baadhi ya mashamba yaliyokutwa na zao hilo haramu.

Zoezi hilo liliongozwa na Kamanda wa polisi wa mkoa wa Simiyu Onesmo Lyanga, pamoja na askari wengi, ambapo Kamanda Lyanga alieleza kuwa zoezi hilo ni endelevu.


Lyanga alieleza kuwa wananchi wengi katika vijiji vinavyopakana na pori la akiba la Maswa wanajihusisha na kilimo hicho, na kuongeza kuwa atahakikisha anapambana na watu wanaojihusisha na kilimo hicho haramu, huku akiwataka wananchi kuachana nacho mara moja na badala yake walime mazao mengine halali.


Angalia Picha hapa chini-Picha zote kwa hisani ya Simiyunews blog


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu (katikati) Onesmo Lyanga akiongoza operasheni hiyo









Kamanda wa polisi Mkoa wa Simiyu Onesmo Lyanga akiongea na vyombo vya habari katika eneo la operasheni hiyo katika kijiji cha Uhusi wilayani Bariadi Mkoani Simiyu.
Moja ya shamba lililokuwa limelimwa Bangi.















Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu Onesmo Lyanga akionyesha waandishi wa habari bangi iliyokuwa ikiteketezwa. 
Chanzo-Simiyunews blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527