Angalia Picha!! Kikao Cha Wadau Wa Mpango Wa Kunusuru Kaya Maskini TASAF Awamu ya Tatu Mkoa wa Shinyanga


Hapa ni ndani ya kumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkaguzi Mkazi mkoa wa Shinyanga ambapo leo Aprili 29,kumefanyika kikao cha Wadau wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini TASAF Awamu ya Tatu mkoa wa Shinyanga unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(Tanzania Social Action Fund-TASAF).
 
 
Lengo la kikao hicho ni kupata ufafanuzi wa miongozo kuhusu utekelezaji wa mpango huo,kujadili changamoto,kupeana uzoefu katika kuzishughulikia na hatimaye kuweka maazimio kwa nia ya utekelezaji wa mpango huo katika mkoa wa Shinyanga.
 
Kikao hicho pia kimehudhuriwa na mkurugenzi wa Uratibu TASAF Makao Makuu Dar e s salaam na mgeni rasmi alikuwa kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Josephine Matiro.Mwandishi wetu Kadama Malunde alikuwepo wakati wa kikao hicho angalia picha hapa chini


Mratibu wa TASAF mkoa wa Shinyanga Maligisa James akiwatambulisha Wadau wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini TASAF Awamu ya Tatu mkoa wa Shinyanga akiwemo mkuguzi mkuu wa nje wa hesabu za serikali mkoa wa Shinyanga,wakuu wa sehemu za afya,elimu na maji,waratibu wa TASAF kutoka halmashauri 6 za mkoa wa Shinyanga,maafisa ushauri na ufuatiliaji,wahasibu wa mpango kutoka mamlaka za serikali za mitaa,wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa na wengine wengi wakiwemo waandishi wa habari


Kushoto ni kaimu katibu tawala mkoa wa Shinyanga Mohammed Iddi Nchira,akifuatiwa na mgeni rasmi/kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Josephine Matiro na mkurugenzi wa Uratibu TASAF Makao makuu Dar es salaam Alphonce Kyariga wakiwa katika kikao hichoWadau wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini TASAF Awamu ya Tatu mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini


Wadau wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini TASAF Awamu ya Tatu mkoa wa Shinyanga wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini


Kaimu katibu tawala mkoa wa Shinyanga Mohammed Iddi Nchira akifungua kikao hicho
Kikao kinaendelea
Kikao kinaendelea


Wajumbe wa kikao hicho wakiandika dondoo muhimu


Tunafuatilia kinachoendelea

Waratibu wa TASAF kutoka halmashauri za wilaya wakiteta jambo ukumbini
Kikao kinaendelea


Wajumbe wakiwa ukumbiniMgeni rasmi ambaye ni kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Josephine Matiro akizungumza katika kikao hicho ambapo alisema shughuli za malipo kwa walengwa wa mpango huo zilizinduliwa tarehe 3 Agosti 2015 na baada ya kufanyika zoezi la utambuzi wa kaya maskini mkoani Shinyanga kaya 542 zilibainika kuwa hazistahili kuwa kwenye mpango huo.

Matiro aliongeza kuwa kaya 34,883 zilibainika kuwa na sifa za kuingizwa katika mpango huo lakini kuna walengwa hewa 542,kati yao 207 ni za manispaa ya Shinyanga na zimeondolewa kwenye mpango wa kunusuru kaya maskini kwa sababu zimeingizwa kimakosa kwani zina hali nzuri kiuchumi


Tunamsikiliza mgeni rasmi


Kaimu mkuu huyo wa mkoa wa Shinyanga pia aliwataka waratibu wa Tasaf ngazi za halmashauri na mkoa kutekeleza majukumu yao vizuri na pale wanapoona kuna tatizo washirikishe viongozi wa halmashauri na mkoa ili kuwatendea haki wananchi huku akiwataka kuwachukulia hatua wanaoingiza walengwa hewa kwenye mpango huo wa kusaidia kaya maskini

Kushoto ni meneja wa fedha kutoka Makao makuu TASAF Godwin Mkisi akiwa na afisa mawasiliano wa TASAF Zabron Bugingo

Mratibu wa TASAF manispaa ya Shinyanga Octavian Kiwone akiwasilisha taarifa ya robo ya tatu 2015/2016 ya mpango wa kunusuru kaya maskini kutoka katika halmashauri hiyo


Mratibu wa TASAF manispaa ya Shinyanga Octavian Kiwone akiwasilisha taarifa yake

Kushoto ni mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna akiwa na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Kiomoni Kibamba
Miongoni mwa changamoto zilizobainishwa na Mratibu wa TASAF manispaa ya Shinyanga Octavian Kiwone katika halmashauri hiyo

Mkurugenzi wa Uratibu TASAF Makao Makuu Dar e s salaam akizungumza katika kikao hicho ambapo aliwataka waratibu wa TASAF na wahusika wote wa mpango huo kuwajibika na kuacha kufanya kazi kwa mazoea


Mkurugenzi wa Uratibu TASAF Makao Makuu Dar e s salaam akizungumza katika kikao hicho
Kikao kinaendelea

Afisa mawasiliano wa TASAF kutoka makao makuu Dar es salaam Zabron Bugingo akiwahamasisha waratibu wa TASAF kushirikiana na vyombo vya habari wakiwa wanatekeleza majumu yao

Kikao kinaendelea

Picha ya pamoja Wadau wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini TASAF Awamu ya Tatu mkoa wa Shinyanga unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(Tanzania Social Action Fund-TASAF)

Wadau wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini TASAF Awamu ya Tatu mkoa wa Shinyanga-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post