Abiria Zaidi 40 Wanusurika Kifo Baada ya Basi Kuacha Njia na Kupinduka Simiyu



Abiria wapatao 40 wamenusurika kifo kufuatia busi walilokuwa wakisafiria kutoka wilayani Bariadi mkoani Simiyu kwenda Ushirombo mkoani Shinyanga kuacha njia na kupinduka. 



Ajali hiyo imetokea majira ya saa 12 alfajili katika kijiji cha Kidurya nje kidogo ya mji wa Bariadi ambapo bus hilo mali ya kampuni ya Luqman aina ya Scania lenye namba za usajili T302 AUU, lilipoacha njia na kupinduka.



Kamanda wa polisi wa mkoa wa Simiyu ,Onesmo Lyanga amethibitsha kutokea kwa ajali hiyo.

Kwa upande wake kaimu mganga mkuu wa hospitali ya mji wa Bariadi, Dr.Saidi Mlowasha amesema amepokea majeruhi watatu ambao wamefikishwa hospitalini hapo na kutibiwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post