WATU 6 WAFARIKI KATIKA AJALI YA BASI KATIKA MLIMA IPOGOLO, 38 WAJERUHIWAWatu sita wamefariki dunia katika ajali iliyotokea katika Mlima Ipogolo baada ya Basi la Lupondije linalofanya safari zake kati ya Iringa na Mwanza kupinduka baada ya mfumo wa breki kushindwa kufanya kazi. 


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Peter Kakamba amesema Dereva wa basi hilo ambalo hufanya safari zake kati ya Iringa na Mwanza alilazimisha kupita na abiria wote wakiwemo waliopaswa kushuka kituo kikuu cha mabasi Iringa ili kuwahi moja ya mabasi yaendayo Mbeya kutokea Dar es Salaam ili afaulishe abiria waliokuwa wanaelekea mkoani Mbeya. 


Abiria wanasema ajali hiyo imetokana na uzembe wa dereva kwani basi hilo lilimshinda na kupinduka.

Katika ajali hiyo jumla ya watu 38 wamejeruhiwa na baadhi yao kulazwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Iringa ambapo 11 kati yao wametibiwa na kuruhusiwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527