RAIS MAGUFULI AWATAKA WAKUU WA MIKOA KUKOMAA NA VIJANA WAZEMBE,WACHEZA POOL TABLE ASUBUHI WATAKIONA CHA MOTO




Rais John Magufuli leo amewaapisha wakuu wa mikoa wapya aliowateua hivi karibuni na katika hotuba yake amewataka wakuu wa mikoa hao wapya kuhakikisha vijana wanafanya kazi na kuacha uzembe.



Rais Magufuli amewataka wakuu wa mikoa hao kuhakikisha hakuna vijana ambao watakuwa wanakwenda kucheza pool table asubuhi na badala yake vijana hao wanatakiwa kufanya kazi kweli kweli hata kwa kulazimishwa.


"Nimeamua kuwateua wakuu wa mikoa nikiamini kwamba mtaniwakilisha vizuri katika mikoa yenu.

"Napenda niwape pole kwa sababu mtakwenda kufanya kazi kweli kweli kutatua kero za wananchi wetu.

"Lakini pia niwaombe wakuu wa mikoa mkasimamie watu wafanye kazi hasa vijana.

"Haiwezekani vijana leo hii unawakuta saa mbili asubuhi wanacheza Pool table wakati wakina mama wanalima shambani, kama hawataki kufanya kazi kwa kupenda walazimishwe kufanya kazi. Atakayekataa mpelekeni kambini akafanye kazi" amesema Rais Magufuli


Rais Magufuli ameongelea pia suala la wafanyakazi hewa kwenye Halmashauri zote nchini ambapo amewapa siku 15 wakuu wapya wa mikoa kuhakikisha hakuna wafanyakazi hewa katika Halmashauri zote nchini.

"Niwape grace time ndani ya siku 15 wakurugenzi wawe wamejumlisha na wamewatoa wafanyakazi hewa katika payroll



"Mshahara wa mwezi tukigundua mkurugenzi amelipa mshahara hewa ajue hana kazi na tunampeleka mahakamani


"Singida na Dodoma ina wafanyakazi hewa 202 wanalipwa mishahara hewa na kwenye data ilionyesha wengine wamefariki, wamestaafu, wamefukuzwa , wengine likizo bila malipo wote hao kumbe wanalipwa malipo ya serikali fedha ambazo zingetumika kutatua matatizo ya wananchi"

"Nimeamua kuwateua nyinyi kama wakuu wa mikoa nikiamini mtaniwakilisha vizuri popote.



"Tusiogope kuchukua maamuzi, nafuu uchukue maamuzi hata kama ni mabaya yatarekebika huko mbele."Amesema Rais Magufuli

==>Kwa habari zaidi tazama video hii umsikilize


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527