Picha!! MBUNGE ESTER BULAYA AWASILI JIJINI MWANZA,BAADA YA KUKAMATWA NA POLISI KUTOKA MWANZA HADI DAR,AISHANGAA SERIKALI

Mbunge wa Bunda mjini.Ester Bulaya amewasili jijini Mwanza usiku huu baada ya kuhojiwa kwa masaa matatu jijini Dar na kikao cha kamati ya haki, kinga na madaraka ya bunge.

Bulaya alikamatwa usiku wa manane wa kumkia Machi 12,2016 kwa amri ya spika wa bunge ambapo alisafirishwa hadi jijini Dar es Salaam kwa ndege kujibu tuhuma zinazomkabili.


Akiongea na waandishi wa habari baada ya kurejea jijini Mwanza usiku huu, Bulaya amesema anashangazwa na kitendo cha serikali kutumia pesa na nguvu nyingi kumkamata wakati pesa hizo zingeweza kutumika kuboresha maisha ya askari polisi

 


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post